ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 18, 2016

TCCIA YAWAALIKA BRELA NA COSOTA KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI MWANZA KUTOA ELIMU YA USAJILI NA HATI MILIKI ILI KUDHIBITI WIZI WA TEKNOLOJIA KWA VIWANDA NA WABUNIFU WETU.

Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema  akizungumza na waandishi wa habari hii leo Jijini Mwanza kuelekea Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agosti 26, 2016 hadi Septemba 04, 2016 katika viwanja vya Rock City Mall.
Milango imefunguliwa kwa Wakala wa Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara nchini (BRELA) pamoja na Chama Cha Haki miliki Tanzania (COSOTA) kushiriki katika Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki  (MEATF) kutoa elimu ya umuhimu wa kuwa na Hatimiliki na Usajili wa makampuni ili kudhibiti makampuni feki, wezi wa teknolojia na kazi za wabunifu wetu nchini.


Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, ametoa rai hiyo leo Jijini Mwanza, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye kusanyiko la utoaji taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza kushika kasi mnamo mwezi Agosti 26 hadi Septemba 4 mwaka huu 2016 katika viwanja vya Rock City Mall.

Lema amesema kuwa wajasiliamali wengi nchini kutokana na kukosa elimu ya umuhimu wa kusajili bidhaa zao, huibiwa ubunifu wao katika utengenezaji wa bidhaa  zinazotoka kwenye viwanda vyao vidogo vidogo, ambapo makampuni mengine hutumia mwanya huo kuiba teknolojia, kuiboresha, wakisajili na kuanza kuzalisha bidhaa hizo wakidai ndiyo waanzilishi, hali ambayo huwanyima haki waanzilishi asilia.

"Ipo haja sasa ya kuwaita BRELA na COSOTA, kushiriki maonesho haya, watumie makusanyiko ya wajasiliamali na wafanyabiashara wa viwanda vidogo kuwapa elimu ili wasiibiwe ubunifu wao" alisema Bw. Leopard Lema,

"Maonesho haya yatasaidia kampuni zetu za Afrika mashariki kuweza kupambana na masoko ya  hadhi za kimataifa kama vile AGOA, EPA, EBA hivyo tunatengeneza mazingira kwa wafanyabiashara wetu kuingia katika hiyo mikataba na kufanya nayo kazi katika ngazi za kimapinduzi"
Wana-habari kazini.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi hii leo Jijini Mwanza kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayotaraji kuanza Agosti 26, 2016 hadi Septemba 04, 2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.

Wengine katika picha ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (wa pili kulia) na Majid Igangula (wa kwanza kulia), kutoka bodi ya Washauri TCCIA.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (kulia), akikazia jambo kuelekea Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayotaraji kuanza Agosti 26, 2016 hadi Septemba 04, 2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza, kushoto ni  Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza Hassan Karambi.
Mwanza East Africa Tade Fair (MEATF) haya ni maonesho ya 11 sasa, ambayo yamekuwa yakitumika kuukuza uchumi wa viwanda vilivyoko Kanda ya Ziwa, nchi kwa ujumla na vile vya nchi za Afrika ya Mashariki.

Tukipata fursa kubwa Mwanza, na sisi wana Mwanza tutaneemeka zaidi kupitia shughulizetu za huduma na biashara zitakuwa kwa kasi.
"Kauli mbiu ya Mwaka huu imesimamia katika Kuongeza biashara kwa wana jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na uwekezaji"  aliweka msisitizo Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza kushoto), 
Kutoka kushoto  walioketi meza kuu ni Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (katikati) na Majid Igangula (kulia), kutoka bodi ya Washauri TCCIA.


This Exhibition aims at achieving the following:-
- To provide an opportunitiy for companies within Tanzania and East African Community to enhance brand and corporate image.

- To provide an opportunity Develop and cultivate customer relation, search for partners and act as market resrarch instrument.

- To tape the opportunity of Mwanza Region as the best available market and Investment area with its excellent strategic location in East Africa.

- To stage this fair as service to the business community as one of the TCCAI'S core objectives.

- To provide an opportunity for Tanzanian Companies to learn and enhance export trade in order to capture available privileged and ready arranged markets worldwide (i.e. AGOA, EPA, EBA etc)

- To give practical support to the East Africans Community integration efforts.
Makampuni mbalimbali na wadau wa sekta binafsi na zile za Serikali tayari yamekwisha thibitisha kushiriki maonesho hayo, zikiwemo idara mbalimbali za Serikali, mifuko ya hifadhi za jamii ambapo kwa ujumla wao ni washiriki zaidi ya 300 toka nchi za Kenya, Uganda, India, China na wenyeji Tanzania.
Maonesho ya mwaka uliopita yalipata takribani wahudhuria wapatao 250,000 toka Kanda ya Ziwa nayo mategemeo kwa mwaka huu ni kupata wahudhuriaji zaidi ya 450,000.

Asilimia kubwa ya Makampuni yote yaliyopo Afrika ya Mashariki kwa msimu wa mwaka 2015-2016 yalihudhuria maonesho yaliyopita ambapo kutokana na manufaa waliyopata msimu uliopita, tayari yameonesha kila dalili ya kutaka kuwemo tena ndani.
Waandishi kazini.
Bidhaa na huduma zisizoruhusiwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Silaha za aina zote, Risasi, Mizinga (Bidhaa za kivita), pamoja na huduma za masuala ya  kisiasa na kidini kwani ni Biashara na Uwekezaji tu ndiyo umezingatiwa na kamati ya maandalizi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.