ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 29, 2016

RADIO 5 NA MAGIC FM VYAFUNGIWA MIDA USIOJULIKANA.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya Redio kurusha matangazo yao.

Waziri Nape ametangaza uamuzi huo hivi punde katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuzitaja redio hizo kuwa ni Radio 5 FM ya Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam.

“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.

Amesema redio hizo kwa nyakati tofauti na katika vipindi vyao tofauti walitangaza habari zilizokuwa na uchochezi ambazo zinaweza kuvuruga amani ya nchi.

Aidha Nape amesema amewasiliana na kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuwahoji wahusika na kisha kushauri adhabu ambazo zitakazofaa dhidi yao.

Source: Habari Leo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.