ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 25, 2016

MORO KIDS WASHINDA Airtel Rising Stars MOROGORO.

Kapteni wa timu ya Moro Kids Abdul Rashid akipokea kombe la mshindi wa kwanza wa mashindano ya Airtel Rising Stars kutoka kwa mgeni rasmi ambae ni Meya wa Manispaa ya Morogoro pascal kihanga, Moro Kids imenyakua kombe hilo baada ya kuifunga timu ya Angrikana 1-0. 

Wachezaji wa timu ya moro kids wakishangilia baada ya kunyakua kombe la mashindano ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ya Angrikana 1-0 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro jana.
Mshambuliaji wa timu ya Angrikana Saidi Mohamed akidhibitiwa kikamilifu na beki wa timu ya Moro Kids Ibrahim Yohana katika pambano la fainali ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo moro kids ilinyakua kombe hilo baada ya kushinda 1-0.
Mchezaji wa timu ya Moro Kids Ibrahimu Ally mwenye jezi nyeupe wakiwania mpira na mchezaji wa timu ya Angrikana Baraka Omary katika mchezo wa fainali ya Airtel Rising Starkwenye uwanja wa Jamhuri Morogoroo. Moro Kids ilinyakua kombe hilo kwa ushindi wa 1-0.
Moro Kids washinda Airtel Rising Stars Morogoro
Timu ya vijana ya Moro Kids imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kufanya kazi ya ziada na kuishinda timu ngumu ya Angrikana 1-0 katika mchezo wenye upinzani mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana.

Goli hilo la ushindi liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Nyamawi Juma katika dakika ya 22 baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Angrikana na kuachia shuti kali lililotinga wavuni. Goli liliibua nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.

Angrikana walijibu mapigo kwa kufanya mashambulizi mfululizo ambayo hata hivyo hayakuweza kuzaa matunda. Kipingi cha pili walikianza kwa matumaini ya kupata goli la kusawazisha lakini hadi dakika ya mwisho matokeo yalibaki kuwa 1-0.

Akikabidhi kikombe kwa washindi, Meya wa manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza Morogoro Kids kwa mafanikio makubwa na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa kujituma huku wakifuata maelekezo ya walimu wao. “Kwa kufanya hivyo kutawaweka katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto zenu za kufanikiwa katika maisha kupitia soka”, alisema.

Aliwataka viongozi wa soka mkoani Morogoro pamoja na makocha kuhakikisha wanachagua vijana wenye vipaji ili kuuwakilisha vyema mkoa wa Morogoro kwenye fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi to 11.
Wakati wa mechi hizo za mkoa makocha walipata fursa ya kuwatathimini uwezo wa kila mchezaji na kuchagua vijana wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa. Mikoa mingine ambayo tayari imeshaunda vikosi vyake ni kwa fainali hizo ni Ilala, Kinondoni, Temeke and Mwanza.

Fainali hizo za kila mwaka itazikutanisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Washiriki wengine watatoka Mwanza, Morogoro, Mbeya, Lindi, Arusha na Zanzibar. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.