ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 29, 2016

MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO NA VIJANA PAMOJA NA KOCHA KUTOKA USA


MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO NA VIJANA (CHILDREN& YOUTH BASKETBALL CLINIC) KUFANYIKA SEPTEMBA KWA KUSHIRIKIANA NA KOCHA GEORGE ELLIS KUTOKA NCHINI MAREKANI HAPA MKOANI MWANZA.
Chama cha mpira wa kikapu mkoani Mwanza (MRBA) kwa kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela(kitengo cha Utamaduni na Michezo) sambamba Planet Social Development (PSD), tunaandaa mafunzo ya siku moja ya mpira wa kikapu kwa watoto na vijana kwa kushirikiana na Kocha George Ellis kutoka nchini Marekani siku ya Jumatatu ya tarehe 12 Septemba 2016.

Mafunzo haya ambayo ni muendelezo wa program ya uibuaji vipaji na mafunzo yanayoendelea katika kiwanja cha mpira wa kikapu Kiloleli, yatahusisha pia makocha kutoka Dar es Salaam na Mwanza ikiwa nao ni sehemu kujifunza namna ya kuendesha mafunzo kama haya kwa watoto na vijana.
Tunatarajia mafunzo haya kufanika katika uwanja wa CCM Kirumba ama Kiloleli, yatajumuisha wanafunzi wanaocheza mchezo huu kutoka katika shule mbalimbali  za msingi na sekondari zilizopo hapa jijini Mwanza kwa maana ya Wilaya ya Ilemela na Nyamagana na pia wachezaji kutoka katika shule mbalimbali.
Coach George Ellis ambae alishawahi kuja hapa Tanzania mwaka jana 2015 na kuendesha mafunzo mbalimbali akiwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa kikapu ya Tanzania, Matthew McCollister, anatarajiwa kufanya mafunzo haya kwa mikoa mitatu kwa kuanza na Dar es salaam, Mwanza na Arusha.
Kwetu sisi tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia kufanikisha mafunzo haya kwa maana ya chakula na malazi kwa Kocha George na makocha watakaotoka Dar,usafiri wa ndani,  maji ya kunywa kwa washiriki, usafiri wa wachezaji wanaotoka pembezoni, jezi na tshirts. 

Bado tuna imani kupata support kutoka kwa wadau na makampuni/taasisi mbalimbali ambao tulikuwa nao wakati wa uzinduzi wa program hii iliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi,  Mheshimiwa Angeline Mabula (MB). Wadau hao ni Mkurugenzi  Manispaa ya Ilemela, CRDB Bank, FNB Bank, The Angeline Foundation, MOIL, Chemi & Cotex Co. Ltd, PEPSI, Atlas Copco na wadau wengine mbalimbali.

Tuna imani hapo baadae wachezaji wa Mwanza watapata nafasi ya kwenda kusoma na kucheza nchini Marekeni kwa maana ya Scholarship endapo watakuwa wanafaulu vizuri katika masomo na kufanya vizuri katika mchezo huu kwani huendana sambamba. Tunataraji Kocha George ataingia hapa tarehe 11 Septemba 2016.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.