ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 21, 2016

UGOMVI WA LAPTOP WASABABISHA POLISI MWANZA KUUAWA.

Askari polisi kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoani Mwanza, Pc John Nyange (G.5092) (pichani), amefariki dunia wakati akikimbizwa hospitalini, baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, kwenye klabu ya Villa Park Resort.

Ameongeza kwamba, mtuhumiwa wa mauaji hayo ametambulika kuwa ni mkazi wa mtaa wa Kigoto kata ya Kirumba aitwaye, Magina Hussein (27), fundi kompyuta ambaye inadaiwa kwamba alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na marehemu uliotokana na marehemu enzi za uhai wake kumdai mtuhumiwa huyo kompyuta mpakato (laptop).

Tayari mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake watano wamekamatwa na jeshi la polisi ambapo uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mbele ya sheria.

Kamanda Msangi amesikitishwa na tukio hilo ambapo amesema jeshi la polisi limempoteza askari kijana ambaye lilikuwa likimtegemea na amewaonya wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kuepukana na vifo vinavyoepukika.

Enzi za uhai wake, askari huyo pia alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi Memorial Universty cha mjini Moshi, akisomea Sayansi ya Habari na Mawasiliano mwaka wa pili na alikuwa Jijini Mwanza kwa ajili ya likizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.