ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 13, 2016

ZIARA RC MWANZA UJENZI WA BARABARA YA MAKONGORO

Mhe. John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiongea na waandishi wa habari mara baada yakufanya ziara ya kukagua barabara ya Makongoro Uwanja wa Ndege inayopanuliwa na Mkandarasi Nyanza Road ya Jijini Mwanza na kutoa maelekezo yakuikabidhi barabara hiyo ifikapo Novemba, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwasili katika Eneo la Ghana tayari kwa ukaguzi wa barabara inayopanuliwa na kujengwa kwa lami kwa kiwango cha Km 2.7.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, akitoa maelekezo kwa Mtaalaam mshauri, namna gani wafanye ili kuweza kuepusha athari ya mafuriko pindi mvua zitakapo nyesha.
Moja ya Mainjinia wa Nyanza Roads works, alipokutwa kazini, wakati wa ziara ya Mhe, John Mongella  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ukaguzi wa barabara hiyo.
Mhandisi wa Maji mjini Mwanza, Mhandisi Sanga, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari namna walivyo tekeleza, maazimio yakuhamisha miundo mbinu ya maji ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo ya makongoro.(Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.