ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 11, 2016

VIPANDE VYA MENO YA TEMBO 666 VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH. BILIONI NNE VYANASWA NA POLISI.

  
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwani Athuman akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijiji Dar es Salaam leo, kuhusu Jeshi la Polisi kutokubali kuona kundi la watu wachache linatishia usalama wa maisha ya raia na mali zao, Wote watakaobainika kuwa ni wahalifu watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi  nchini kwa kishirikiana na Ofisi za Interpol Kanda ya Kusini Mwa Afrika imefanya operesheni  na kukamata vipande vya meno ya Tembo 666 vyenye uzito wa Kilogram 1279.19 vyenye thamani zaidi ya a Sh. Biloni Nne.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa  Jeshi  la Polisi (CP), Diwani Athuman wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa vipande hivyo vya tembo yamehusisha watu tisa  kati yao mmoja ni Raia wa Guinea na mwingine ni Raia wa Uganda.

Amesema kuwa katika operesheni Usalama  III wameweza kukamata  vitu mbalimbali kutokana na taarifa za kiitelijensia zilizokusanywa wakati wa matayarisho ya operesheni ya Usalama III, ambapo waliweza kukamata mitambo ya 18 ya kutengenezea gongo pamoja na  lita  za gongo  960  zimekamatwa.

Athuman amesema katika Operesheni  hiyo wameweza kukamata watuhumiwa 265  ambapo baada ya uchunguzi wataobainika  kuhusika na  vitendo vya kihalifu watafikishwa mahakamani mara moja ikiwa namna au nyingine katika kufankisha vitendo vya kihalifu.

Kamishina Othman amesema ametoa rai kwa wanunuzi wa magari nje ya nchi kuwasiliana na ofisi za Interpol za ndani au nje ya nchi magari yanakotoka kwa uchunguzi kabla ya kuyanunua ili kuondoa usumbufu wa kukamatwa mara kwa mara katika operesheni  kama hizi.

Amesema kutokana na operesheni hiyo jeshi la polisi halitakubali kuona kundi la watu wachache linalotishia usalama maisha raia wema na  mali zao na wataobainika kufanya hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria bila kusita.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.