ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 7, 2016

URENO YATINGA FAINALI EURO 2016 KWA KUICHAPA KIRAHISI WALES HUKU RONALDO AKIVUNJA REKODI.Usiku wa July 6 2016 michuano ya mataifa ya Ulaya 2016 maarufu kama Kombe la Euro, ilirejea tena baada ya kusimama kwa siku mbili kwa ajili ya mapumziko, usiku wa July 6 2016 ulichezwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Euro 2016 kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ureno dhidi ya Wales.


Katika mchezo huo Ureno ambayo mara ya mwisho kufungwa na Wales ilikuwa May 12 1951 katika mchezo wa kirafiki, ilifanikiwa kuitoa Wales kwa kuifunga jumla ya goli 2-0, magoli ya Ureno yalifungwa kuanzia dakika ya 50 na Cristiano Ronaldo kwa kichwa.
Gooooooooooooo......!!!!

Baada ya bao la CR dakika 3 baadae Luis Nani akapachika goli la pili kwa kutumia vyema assist ya Ronaldo.

 Kwa ushindi huo Cristiano Ronaldo ambaye ndio mchezaji bora wa mechi, anakuwa amefikia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote iliyokuwa inashikiliwa na Michael Platini ya kufunga jumla ya magoli 9, Ronaldo ana nafasi ya kuvunja rekodi hiyo kama katika mchezo wa fainali atakaocheza na mshindi kati ya Ufaransa na Ujerumani kufunga goli moja.

IFUATAYO NI TATHIMINI YA MCHEZO HUO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.