ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 2, 2016

SASA NI VITA KATI YA CHRISTIANO RONALDO DHIDI YA GARETH BALE.

TIMU ya soka ya Wales iliweka rekodi nzuri usiku wa Jumamosi katika historia ya soka nchini humo walipotoka nyuma na kuishinda Ubelgiji katika michuano ya Euro 2016 na hivyobasi kujikatia tiketi ya nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mchuano mkubwa.

Radja Nainggolan aliiweka kifua mbele Ubelgiji mjini Lille kupitia mkwaju mkali alioupiga umbali wa miguu 25 lakini nahodha wa Wales Ashley Williams alifunga bao la kichwa kupitia kona na kusawazisha katika kipindi cha kwanza cha mechi.
Lakini mashabiki wa Wales walifurahishwa zaidi na bao lililofungwa na Hal Robson Kanu ,ambaye ni mshambuliaji bila klabu,na kufanya mambo kuwa 2-1.
Na baada ya presha kali kutoka kwa washambuliaji wa Ubelgiji ,Wales walikifunga kidomodomo cha wapinzani wao kupitia kichwa kilichofungwa na mchezaji wa ziada Sam Vokes na hivyobasi kutinga nusu fainali dhidi ya Ureno huku wachezaji nyota wa Real Madrid Gareth Bale na Christiano Ronaldo wakijipata katika pande pinzani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.