ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 19, 2016

SAFARI YA MWISHO YA MWANAHABARI + MWANAMUZIKI + MTUMISHI CHARLES SOKOLO

Mwili wa aliyekuwa Mwanahabari, Mwanamuziki na vilevile mwimbaji wa Kwaya ya AICT Makongoro Mwanza Charles Sokoro, umeagwa leo katika Kanisa la AICT Makongoro Jijini Mwanza na baadaye mazishi yamefanyika katika makaburi ya Kitangiri majira ya saa kumi jioni.
Mke wa marehemu pamoja na ndugu jamaa na marafiki wamekuwa katika kipindi kigumu hii leo wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Charles Sokoro ambaye pia alikuwa Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Barmedas Mwanza.
Mtoto wa kwanza wa marehemu akiuaga mwili wa mpendwa baba yake.
Askofu mstaafu Nyagwaswa akiongoza msafara wa Ma-Askofu na Wachungaji katika kutoa heshia za mwisho kwa mwili wa marehemu Charles Sokoro, katika ibada iliyofanyika katika kanisa la AICT Makongoro Mwanza leo.
Mwanahabari kutoka gazeti la Mtanzania Peter Fabian akitoa heshimma za mwisho kwa mwii wa marehemu Charles Sokoro,
Mwanahabari Mansour Jumanne kutoka Jembe Fm akiongoza msafara wa wanahabari wengine kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Charles Sokoro, ambaye amezikwa leo alasili katika makaburi ya Kitangiri wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Atley Kuni na heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Charles Sokoro.
Mama Simbira.
"Tangulia Mwalimu"
Familia ya merehemu Charles Songora.
Wanafunzi wake pamoja na wafanyakazi wenzake........
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) Joseph Songora ndiye aliyekuwa Mc wa shughuli za ibada ya heshima kanisani na hapa akiwa mbele ya mwili wa marehemu akitoa heshima za mwisho.
Kwaya aliyoitumikia marehemu enzi za uhai wake.
Shukuruni kwa kila jambo.
Marehemu Charles Sokoro alizaliwa tarehe 01/July/1965 na mnamo tarehe 16/July/ 2016 ndipo alipo fikwa na mauti. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mwili wa aliyekuwa Mwanahabari Charles Sokoro ukitoka katika kanisa la AICT Makongoro mara baada ya ibada kumalizika na sasa tayari kwenda kwenye nyumba yake ya milele.
Lango kuu la Kanisa la AICT Makongoro.
Nenda rafiki.
Wanahabari mbele ya nyumba ya milele ya mwanahabari Charles Sokoro.
Kwa heri ya kuonana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.