ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 21, 2016

RAPPER KEKO ASEMA ALIKIBA NI MSANII ALIYEINSPIRE STYLE YA DIAMOND.



Rapper wa nchini Uganda, Keko amedai kuwa alianza kumsikiliza Alikiba tangu akiwa high school na anaamini kuwa ni msanii aliyeinspire style ya Diamond.

Keko amesama hayo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

“Nimekuwa nikimsikiliza Alikiba tangu nikiwa high school, nadhani alianzisha mtindo ambao Diamond anao pia,” alisema.

“Na sijaribu kuleta mgogoro lakini naamini Alikiba alianzisha style hiyo na hongera kwa meneja wake kwa kufufua career yake jinsi ambavyo imepamba moto sasa hivi,” aliongeza.

Keko pia alisainishwa kwenye label ya Sony Music miaka kadhaa iliyopita japo amekuwa na maelewano kidogo na uongozi wake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.