ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 4, 2016

PICHA: AJALI YAUA WATU 24 NA KUJERUHI WENGINE MKOANI SINGIDA LEO...



Taarifa iliyotufikia chumba chetu cha habari muda huu, inaeleza kuwa ajali mbali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria, imetokea katika eneo la Manyoni Mkoani Singida na kupelekea vifo vya abiria 24 papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa. 


Akizungumza kwa njia ya simu kuelezea ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nane mchana wa leo, ambayo inayahusisha mabasi ya Kampuni moja ya CITY BOYS ambalo moja lilikuwa likitoka Dar kwenda Kahama huku lingine likitoka Kahama kuelekea Dar.
Na Hizi Ni Baadhi ya PICHA:





Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.