ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 5, 2016

NEMC YASIMAMISHA UJENZI KITUO CHA MAFUTA CHA LAKE OIL MWANZA.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira NEMC limesimamisha ujenzi wa kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo Igogo jijini Mwanza ambacho kilikuwa kinajengwa usiku kwa usiku baada ya wamiliki wake kukaidi agizo la NEMC la kuzuia kuendelea kwa ujenzi wa kituo hicho.
Kituo hicho kilichopo kwenye makutano ya barabara ya Pamba na Kenyata mara ya mwisho kilifungwa juni 27 mwaka huu na Ofisa Mazingira Mkuu wa NEMC Dr.Yohana Mtoni lakini ujenzi huo umekuwa ukiendelea kimya kimya hususani nyakati za usiku jambo ambalo mkuu huyo wa idara ya ukaguzi wa NEMC amedai ni ukiukwaji mkubwa wa sheria no 20 ya mwaka 2004 inayokataza kufanyika kwa shughuli zozote kwa miradi inayohusisha vituo vya mafuta kutojengwa hadi tathimin ya athari kwa mazingira kutolewa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Matiku Mahende ambaye ni balozi  wa mtaa wa Kambarage Igogo akionyesha madhara yaliyojitokeza kwa nyumba zilizo juu kwenye vilima vya igogo ukingoni mwa kituo hicho ambapo katika majira haya ya joto jua litapiga lakini haijajulikana hatma yake kipindi cha mvua hasa mvua kubwa za masika ambazo huambatana na upepo mkali na ngurumo za radi.
BOFYA KUSIKILIZA YANAYOWASIBU.

Hii ni nyumba iliyoko juu kwenye vilima hivi ambayo nayo iko katika hatihati kwani ni moja kati ya zile zilizoko kwenye kingo ya mlima sasa kwa muonekano mara baada ya sehemu ya mlima huo kumegwa na sehemu yake ya ardhi chini kutumika kama sehemu ya kiwanja cha Kituo cha mafuta cha Lake Oil jijini Mwanza.
Kutoka moja ya kuta za nyumba ukingoni mwa vilima hivi vya Igogo, ardhi ikiendelea kupuputika nao wajenzi wa kituo wakiwa wamekinga udongo unaoporomoka kwa kutumia mabati.
Ibrahim Shahban ni mkazi wa maeneo haya akionyesha moja ya barua zilizopuuzwa awali toka Baraza la Ardhi na makazi Igogo.
Kwa ukaribu zaidi.

Baada ya udongo na mawe kuanza kuporomoka hivi ndivyo muwekezaji alivyo weka kingizo za mawe yaliyofungwa na waya kuzuia, ingawa hazifui dafu hasa kipindi cha mvua.


Mwanasheria Mkuu wa NEMC Manchare Suguta amesema sheria kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya watu wanaokaidi maagizo ya Serikali huku akibainisha kwamba hiyo ni mara ya 3 kwa uongozi wa Kampuni hiyo kushindwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa awali. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.