ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 6, 2016

MWANZA NA SIKUKUU YA EID MUBARAK.

Watoto wakielekea ibadani.
Hii leo wakazi wa Mwanza wamejumuika na mamilioni ya waislamu duniani kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri kunako misikiti mbalimbali.
Harakati za kuiwahi ibada ya asubuhi.
Eneo la Kirumba kumekuwa na safari za hapa na pale kwa waumini kutoka kwenye makazi yao na kuelekea sehemu za makusanyiko.
Watoto wa kike kwa waume nao wamehudhuria ibada zilizokuwa zikiendeshwa ndani ya misikiti kadhaa na hawa ni watoto waumini wa dini ya kiislamu toka ndani na nje maeneo ya karibu na kata ya Kirumba ambako kuna msikiti mashuhuri ujulikanao kama Masjid Shamsiyat unaomilikiwa na BAKWATA.
Mara tu baada ya ibada kumalizika ilikuwa ni fursa kwa marafiki kujadili haya na yale nje ya eneo la msikiti.
VIDEO NA SALAMU ZA WADAU.
Wadau wa Gsengo Blog Ramadhan (L) na Samadu Abdul (R)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.