ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 2, 2016

MSIMU WA WACHEZI KUVUNA NDIYO HUU.

KLABU ya Liverpool imekamilisha rasmi usajili wa Sadio Mane aliyetua Anfield kwa kitita cha paundi milioni 34 kutoka Southampton. 

Nyota huyo anajiunga kwa mkataba wa muda mrefu na usajili wa tatu kwa Liverpool kiangazi hiki baada ya kuwa tayari wamewanasa kipa wa kimataifa wa Ujerumani Loris Karius na beki wa Cameroon Joel Matip.

 Ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 24, inadaiwa inaweza kupanda na kufikia paundi milioni 36 hivyo kupita ile ya paundi milioni 35 aliyosajiliwa Andy Carroll mwaka 2011 na kuwa mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo. Mane amefunga mabao 21 katika mechi 67 za Ligi Kuu alizoichezea Southampton baada ya kujiunga nao kwa kitita cha paundi milioni 10 akitokea Salzburg mwaka 2014.

Henrikh Mkhitaryan, 27, atakamilisha uhamisho kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United weekend hii.

Mchezaji huyo kutoka Armenia atagharimu takriban pauni milioni 26 (Daily Mail), Manchester City wapo tayari kulipa hadi pauni milioni 50 kumsajili beki John Stones, 22, kabla ya kuanza kwa mechi za kabla ya msimu (Telegraph), Crystal Palace wamekubali kulipa pauni milioni 12.5 kumsajili beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Daily Mail), mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanafikiria kumsajili beki wa kati wa Arsenal, 30, ambaye mkataba wake Emirates unamalizika mwaka 2019 (Evening Standard),

Everton wamekubali kumsajili kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel, 27, kutoka Zenith St Petersburg na watamlipa mchezaji huyo zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki (Squawka), Stoke City wametoa dau la pauni milioni 16 kutaka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, na wako tayari kumlipa pauni 70,000 kwa wiki (Mirror).

Burnley wanataka kumfanya beki Michael Keane, 23, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ili kuzuia kusajiliwa na Leicester City (Mirror), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 32, anauzwa na klabu yake ya Fernabahce (Evening Standard), mshambuliaji wa Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya na atafanya vipimo West Ham (Manchester Evening News).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.