ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 13, 2016

Mr NICE ASAINI MKATABA MNONO KENYA, ATAFANYA SHOW 51 KATIKA TAMASHA LA ‘47 County Tour’

WhatsApp-Image-20160712


Msanii mkongwe wa muziki nchini, Mr Nice amepata shavu nchini Kenya la kuingia mtakaba na kampuni ya Soko Bay INT LTD ya nchini Kenya kwa ajili ya kufanya show 51 katika tamasha la ‘47 County Tour’. 

Akiongea  Jumanne hii akiwa nchini Kenya, Mr Nice amesema mkataba huyo ni mnono kwake kuwahi kutokea.
“Ni mkataba mnono zaidi kuwahi kutokea kwangu nawashukuru Wakenya kwa kuendelea kuniamini na kunipenda, ni mkataba wa mwaka mmoja ambao ndani yake una kila kitu,” alisema Mr Nice.
Aliongeza,“Ni mkataba wa mwaka mmoja, so ndani ya mwaka mmoja show ni nyingi sana, na nimehakikishiwa angalau show moja every weekend, na kama unavyojua huku wenzetu burudani ni kila siku haina Jumatatu wala weekend but uhakika ni angalau show moja kila wiki lazma iwepo na itakuwa ni tour ya nchi nzima ya kenya na ndiyo maana imepewa jina la 47 County Tour,”
Muimbaji huyo amesema tayari ameshakabidhiwa apartments ya kukaa ambayo alihaidiwa katika mkataba.
Pia amesema Alhamisi hii wanatarajia kwenda ubalozi ya Tanzania uliopo nchini humo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu kuhusu mkataba huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.