ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 20, 2016

MKAZI WA MLANDIZI KIBAHA PWANI APATA UPOFU BAADA YA KUMEZA DAWA AINA YA FANSIDER AOMBA MSAADA ML.18

Dada wa Seleman Mgoto Luiza Mdachi wakati aliozungumza na waandishi kuhusiana na matatizo aliyiyapata kaka yake ya kupoteza kabisa uwezo wa kuona na jinsi familia yake ambayo ipo katika wakati mgumu.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Seleman Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa macho yake mawili baada ya kutumia dawa hizo wakati akizungumza na waandishi kuhusina na changamoto aliyonayo na kuomba msaada kwa wadau mbali mbali kuweza kumsaidia.

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI  

MKAZI mmoja ajulikanaye kwa jina la Seleman Mgoto (42)anayeishi katika kitongoji cha Janga kilichopo eneo la Mlandizi  Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ameathirika macho yake mawili na kupoteza kabisa uwezo wa kuona  baada ya kutumia dawa ya kutibu malaria  aina ya Fansider  hivyo anahitaji msaada wa kiasi cha shilingi milioni 18 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi  nchini India.

Hayo yamebainika baada ya mwandishi habari hizi  kuweza kufika nyumbani  kwa kaka yake maeneo ya mlandizi ambapo ndipo anapoishi kwa sasa baada ya kupatwa na tatizo hilo na kuweza kuzungumza naye kuhusiana na mkasa wa tukio hilo lililompata.

Akizunguza kwa  masikitiko makubwa  Mgoto alisema kwamba mnano  agosti  2012 alikuwa anaumwa  na alipokwenda kupimwa aligundulika kuwa na wadudu tisa  wa ugonjwa wa malaria ndipo alipoandika dawa aina ya fansider na kuamua kwenda kuzinunua katika moja la duka la madawa lililopo maeneo hayo ya mlandizi na baada ya kuzimeza hali yake baada ya siku mbili ilianza kubadilika kutokana na sumu  kali iliyokuwepo mwilini mwake  .

“Mimi mwezi agosti mwaka 2012 ndugu zangu waandishi niliweza kuumwa na nilipoenda kupima afya niligundulika nina malaria, na baada ya hapo niliweza kuandikiwa dawa na nikaenda kununua dawa aina ya fansider, ila baada ya siku mbii hali yangu iiweza kubadilika na nilipokwenda kituo cha afya niilazwa kwa ajili matibabu zaidi,”alisema.

Aidha akifafanua kuhusina na kuangaika katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya matibabu alisema kwamba mara ya mwisho alikwenda kuwaona madaktari bingwa wa hospitari ya CCBRT ya jijini Dar es salaam ambapo walimwambia macho yake kwa hapa Tanzania hayawezi kutibiwa mpaka aende nchini India ndio yanaweza kupona.

Pia katika hatua nyingine amesema kwamba kwa sasa maisha yake yamekuwa ni magumu sana kutokana na kutokuwa na kipato chochote kile anachokiingiza ukizingatia ana familia mke pamoja na watoto watatu ambao wanamtegemea kwa kila kitu ambapo watoto wengine  wawili wapo wanasoma sekondari hivyo kunahitajika mahitaji mengine ya msingi.

Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kumsaidia  kwenda kupatiwa matibabu nchini India Eria Chaofu pamoja na Luiza Mdachi ambaye ni dada  yake  wamesema kwamba familia   imeangaika kwa hali na mali  kwa kipindi cha miaka mitatu katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya  kumtibia bila ya kupata mafanikio yoyote kutokana  na kutokuwa na uwezo wa kifedha. miaka mitatu.

Aidha Mwenyekiti huyo amemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Mgufuli kumsaidia mgonjwa huyo pamoja na wadau wengine wakiwemo wakuu wa wilaya, wabunge, wakuu wa miko pamoja na Wizara ya afya ili aweze kwenda kutibiwa na kurudi katika hali.

 Kwa  mtu yoyote ambaye ameguswa na anahitaji kumsaidia mchango wake  kwa hali na mali  Seleman Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa wa macho yake mawili,atume  kwa tigo pesa -0655-413939 au M-PESA 0754-413939 na akaunti namba NMB -80110000915 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini India kwani zinahitajika shilingi milioni 18.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.