ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 4, 2016

MJUE KINDA MICKY BATSHUAYI ALIYESAJILIWA NA KLABU YA SOKA YA CHELSEA.
Chelsea wameshamsajili mshambuliaji Michy Batshuayi kutoka Marseille kwa mkataba wa miaka mitano.

Kijana huyo mbelgiji wa miaka 22 anakuwa wa kwanza kununuliwa na meneja mpya pale Stamford Bridge.

Antonio Konte. Malipo hayajawekwa wazi lakini inaaminika kuwa ni pauni milioni 33 sawa na Euro milioni 40.

Haya ni Maelezo mafupi kuhusu mchezaji huyo aliyesajiliwa na Chelsea. 

Mitchy Batshuayi Tunga 22 ni mshambuliaji wa Belgium mwenye asilia ya kikongo anayechezea klabu ya Marseille nchini Ufaransa. Kwa sasahivi Mitchy Batshuayi yuko nchini Ufaransa akijaribu kuisaidia nchi yake Belgium kutwaa taji la michuano ya Euro 2016. Mitchy Batshuayi alifunga goli kwenye mechi ya mwisho ya Belgium walioshinda 4-0, lilikuwa goli lake la tatu kwenye mechi 6 tu kwa ajili ya nchi yake.
Mitchy Batshuayi ni mmoja ya wachezaji wanaosakwa na klabu nyingi sana duniani hasa ukizingatia kwamba klabu yake ya Olympique Marseille imeshatangaza kwamba hawategemei mchezaji huyu kurudi kwenye klabu yao kwani wanahitaji kumuuza ili wapate fedha.
Batshuayi alizaliwa Brussels Ubelgiji, na alijitambulisha kwa dunia kwenye klabu ya Standard Liege. Wakati bado kijana mdogo tu, Batshuayi aliisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa ligi ya Belgium msimu wa 2013-2014 akiwa na miaka 21 tu kwa kufunga magoli 21 katika mechi 34.
Katika dirisha kubwa la usajili msimu huo, huku klabu nyingi za Ulaya zikiwa zinamuangalia (hadi Tottenham ambao bado wanaendelea kumkodolea macho), alisajiliwa na klabu ya Marseille kwa kiasi cha Euro millioni 6 tu.
Rekodi yake ya magoli kwenye Ligi ya Ubelgiji ilimuwezesha kuitwa kwenye kikosi cha awali cha Belgium cha Kombe la Dunia la 2014, ila kwa bahati mbaya jina lake lilikatwa kwenye kikosi cha mwisho.
Batshuayi alianza polepole kwenye klabu ya Marseille kwa sababu aikuwa nyuma ya mshambuliaji wa Ufaransa  Andre Pierre Gignac  kwa mda mrefu kwenye msimu. Licha ya kuanza mara 6 tu katika mechi 26 Batshuayi  bado aliweza kufunga magoli 9.
Msimu huu licha ya kusuasua kwa klabu yake ya Marseille, Batshuayi aliweza kufunga magoli mengi sana na takwimu zake zilikuwa kati ya takwimu bora zaidi za washambuliaji wadogo duniani.
Batshuayi alifunga magoli 17 kwenye ligi akimaliza nyuma ya Zlatan Ibrahimovic, Alexander Lacazzete na Edinson Cavani kwenye orodha ya wafungaji bora kwenye ligi ya Ufaransa.
Aliweza kuongeza magoli mengine manne kwenye mechi 6 tu za Europa League na matatu mengine kwenye kombe la Coupe de France na kufikisha idadi yake kuwa magoli 24 kwenye msimu.
Batshuayi anauwezo wa kucheza kama mshambuliaji pekee ama kwenye mfumo wa washambuliaji wawili na hiki ni kitu ambacho kinaweza kuisaidia Chelsea hasa pale Antonio Conte atapoamua kujaribu mfumo wake maarufu wa washambuliaji wawili atapochukua majukumu yake baada ya Euro 2016.
Katika nusu ya pili ya msimu uliopita katika klabu ya Marseille, Batshuayi aliwekwa mbele na mshambuliaji wa Sunderland aliyekuwepo Marseille kwa mkopo Steven Fletcher na wachezaji hawa walijenga uelewano mzuri.
Inaonekana Batshuayi pia ana uwezo wa kutengeneza magoli kwani licha ya magoli yake 17 ya Ligi alitoa pasi za mwisho ama ‘assists’ 9 vilevile.
Batshuayi ameongezeka urefu kidogo na ameongeza mwili wake kwa kiasi kikubwa katika miaka miwili hii. Ana kasi ya ajabu, mwepesi na pia anaweza kuchezea miguu yake yote miwili. Wengi wanamfananisha na Lukaku.
Zamani Batshuayi alikuwa akijulikana kama mchezaji mchoyo lakini hiki si kitu kibaya kwa mshambuliaji. Hii ni kwa sababu Batshuayi alikulia kwenye mitaa ya mji wa Brussels jambo ambalo linamfanya aonekane kama mtukutu lakini tusisahau kwamba kitu hiki kimemuwezesha kufahamu mpira wa mtaani ambao si rahisi kumfundisha mchezaji.
Kama Chelsea wakikamilisha usajili huu Batshuayi anaweza kuwasaidia Chelsea kwa kiasi kikubwa kwani sio siri kama Chelsea wanahitaji mshambuliaji mwingine wa kumpunguzia mzigo Diego Costa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.