ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 13, 2016

MBUNGE WA EAC HAFSA MOSSI AUAWA NCHINI BURUNDI.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.
Bi Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Msemaji wa rais wa Burundi Bw Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo #Bujumburaya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa #EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na #EAC,” ameandika kwenye Twitter.
CHANZO: BBC SWAHILI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.