ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 21, 2016

KERO:- MAKABURI YA KITANGIRI YAGEUZWA DAMPO LA TAKA.

Mtangazi wa kipindi cha 'Kazi na Ngoma' kupitia Jembe Fm Mansour Jumanne (kulia) akifanya mahojiano na mmoja wa wananchi wa jiji la Mwanza baada ya kujionea hali ya mazingira machafu ya makaburi ya Kitangili.
Baadhi ya wananchi wa jijini Mwanza wameilalamikia Halmashauri ya wilaya ya Ilemela kwa kushindwa kuweka utaratibu wa kuyalinda maeneo ya makaburi ya eneo la kata ya Kitangili baada ya baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kugeuza sehemu hiyo kuwa dampo la kutupia taka.

Aidha wananchi hao wameziomba mamlaka husika kuweka kanuni na sheria za kuhifadhi na kulinda maeneo ya makaburi hayo ambayo sasa yamegeuka kuwa eneo la uharibifu mkubwa wa kimazigira.Wakitoa malalamiko yao baadhi ya wakazi wanao fika viwanja hivyo kwaajili ya kuzika ndugu zao wanasema kuwa maeneo hayo ya makaburi yamekuwa yakitoa harufu mbaya baada ya kugeuzwa kuwa dampo la utupaji wa taka , eneo la malishio ya wanyama, kificho cha wezi na waporaji pamoja na akinadada poa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao nyakati za usiku. 

Wamesema licha ya wananchi kulipa fedha ili kuweza kupata eneo la ardhi kama idhini ya kuzika kila mwili wa ndugu au jamaa wanaofariki dunia lakini bado Halmashauri husika imelifumbia macho suala la kuweka uzio kuzunguka eneo la makaburi ikiwa ni sanjari na kuweka walinzi, suala ambalo sasa linawapa kiburi wananchi kufanya wanavyotaka. 


BOFYA PLAY KUSIKILIZATupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.