ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 9, 2016

IVO MAPUNDA NA TAULO LAKE KUREJEA LIGI KUU KENYA.

Baada ya kutokuwa na misimu kadhaa yenye mafanikio akichezea vilabu vya Simba SC na Azam FC za Tanzania kipa maarufu nchini ambaye aliwahi kudakia timu ya Yanga SC Ivo Mapunda huenda akarejea nchini Kenya ambako alipata umaarufu akiwa na Gor Mahia.

Kipa Ivo Philip Mapunda aliyemaliza mkataba wake katika klabu ya Azam FC amesema anaimani rekodi aliyoiacha nchini Kenya misimu kadhaa takribani miaka mitatu iliyopita akiwa na mabingwa wa nchi hiyo Gor Mahia maarufu kama Ingwe itambeba katika harakati zake za kusaka maisha mapya katika soka nchini humo.

Ivo ameanza mikakati mizito ya chinichini ili kurejea nchini humo ambako alipata umaarufu mkubwa akidaka huku akiwa na taulo kubwa golini baada ya kumaliza mkataba wake na Azam FC waliomsajili kutoka klabu ya Simba na klabu hiyo kutangaza kutomwongezea mkataba mpya huku ikishusha makipa wawili wakimataifa toka Hispania na Ivory Coast ambao tayari wameanza majaribio na timu hiyo katika viwanja vya Chamazi jijini Dar es Salaam.

Aidha Mapunda mzaliwa wa jiji la Mbeya mwenye asili ya Songea ambaye kabla ya kutua Gor Mahia alianza maisha ya soka nchini Kenya akiwa na klabu ya Bandari ya Mombasa aliyojiunga nayo akitokea kwa mabingwa wa Tanzania Yanga SC amesema mipango yake ya kwanza ni kurejea kucheza ligi kuu ya Kenya ambayo kwa sasa bado inaendelea ila kwa kipindi hiki anataraji kujisajili kwa timu ambayo itampa kandarasi [mkataba] ya muda mfupi.

Akimalizia Mapunda amesema yeye bado anauwezo mkubwa kama awali na umeongezeka mara dufu na kimsingi kuwekwa benchi katika klabu ya Azam si kwamba uwezo wake ulikuwa mdogo ila ni mipango ya kocha wa timu hiyo kuamua mtumia zaidi kipa kinda mwenye kipaji kikubwa Aishi Manula na yeye na mwenzake Mwadini Ally kubadilishana benchi wakati kinda huyo aliyeibukia katika michuano ya Uhai Cup akitamba mpaka katika timu ya taifa Stars.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.