ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 25, 2016

HASSANOO AWATAKA WAAMUZI WA MCHEZO WA SOKA WAZINGATIE SHERIA 17 NA KUACHANA NA TAMAA.

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAAMUZI wa mchezo wa  soka mkoani Pwani wametakiwa kuhakikisha wanachezesha kwa kuzingatia sheria 17 za mchezo huo na kutoa maamuzi yaliyo sahihi ili wasiwe ni moja ya chanzo cha susababisha migogoro na kuvunjika kwa baadhi ya michezo wanayokuwa wakichezesha.
Kauli hiyo imetolewa na na Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoani Pwani (COREFA) Hassan Hassanoo wakati alipokuwa  akifungua mafunzo kwa waamuzi wa mchezo wa soka wa mkoa huo ambayo yaliyofanyika kwenye  uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha  Tumbi.
Hassano alisema kwamba mwamuzi  wa mchezo wa mpira ni sawa na  na hakimu ambaye anapaswa kutoa maamuzi yake kuzingatia sheria kanuni pamoja na taratibu zote ambazo zimewekwa katika kuongoza mchezo wa soka ii kuweza kutimiza malengo ya kuweza kuuendeleza zaidi kuanzia ngazi za chini hadi za juu.
“Mimi kikubwa ninachowaomba waamuzi katika Mkoa wa Pwani tuwe makini sana katika kutimiza majukumu yenu, kwani wakati mwingine michezo imekuwa ikivunjika na wengine kutoa malalamikoi, kwa hiyo katika hili hakikisheni mnasimamia sheria zote 17 za mchezo huu wa soka katika Mkoa wetu wa Pwani na sio vinginevyo,”alisema Hassanoo.
Aidha aliongeza kuwa suala la kuwa mwamuzi wa mchezo wa soko ni wito na  si suala la  biashara kama baadhi yao wanavyofanya kama sehemu ya kujiongezea kipato kwani mwamuzi anapaswa kuhakikisha mchezo unakwisha salama na hata kama unavunjika sababu iwe ambayo ni nje ya uwezo lakini siyo kusababishwa na mwamuzi.
“Kwa hiyo waamuzi mnapaswa kujifunza kila mara kwa sababu sheria za soka hubadilika kila mara ambapo kwa sasa zimekuwa zikibadilika kama fasheni kwa lengo la kuongeza ladha ya mchezo wa soka hivyo lazima muendane na mabadiliko ya sheria hizo ili kupunguza lawama ambazo zimekuwa zikitolewa ,” alisema Hassanoo.
Aliwataka waamuzi  wasibweteke na madaraja waliyopo bali waongeze bidii ili wafike madaraja ya juu na kuweza kuchezesha ligi kuu kama walivyo baadhi yao na waweze kufikia kuchezesha michezo inayoandaliwa na Mashirikisho ya Soka Afrika CAF na Dunia FIFA na mkoa utaendelea kutoa mafunzo mbalimbali.

Kwa upande wake mmoja ya waamuzi ambaye alisoma risala ya waamuzi hao Kasule ambogo alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolipwa posho zao kwa wakati ambapo zamani walikuwa wakilipwa hata kabla ya mchezo.
Ambogo alisema kuwa pia changamoto nyingine ni kukosa mafunzo hayo ya kujikumbusha sheria za soka kwa muda mrefu hivyo kusababisha waamuzi kushindwa kupanda  madaraja kwa wakati na kuksa hata sifa za kuweza kuchezesha katika ligi kuu ya Tanzania bara.
KOZI hiyo ambayo ilifanyika kwa siku mbili kwa kuwashirikisha waamuzi  wapatao 60 kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Pwani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.