ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 5, 2016

DK KIGWANGALLA AFUNGA RASMI SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 50 YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ILEMELA MWANZA

DSC_9304
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti ya bluu) akiwa katika jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za watu binafsi zikiwemo zile za kidini na kijamii katika kufanikisha maendeleo ambapo amelipongeza Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ilemela Jijini Mwanza kwa hatua yake kujenga Hospitali ya Kisasa ambayo itakuwa msaada katika Wilaya hiyo.

Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la ufungaji wa sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Akitoa hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.
DSC_9310

Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.

“Uwepo wenu tunaupongeza kwani naamini mumekuwa mstari wa mbele katika kuliombea Amani Taifa hili na pia kuwaombea ulinzi watu mbalimbali pamoja na kutoa misaada, huduma za Afya na mambo mengine mbalimbali. Hii ni faraja sana na Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.

Aidha, katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wote.

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo ikiwemo suala la ushoga.

“Serikali haipo tayari kuona vitendo vya ushoga vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangaza kwa jamii. Wizara yangu itakutana na NGOs, zote za Kijamii na taasisi zilizosajiliwa ambazo pia zingine zipo chini ya Wizara yetu kukaa nazo na kujua ni zipi zinajihusisha na masuala haya iwe kwa kutetea ushoga ama kubariki vitendo hivi, tutawachukulia hatua kali za kisheria na hata kuzifuta kabisa” alimalizia Dk. Kigwangalla.

Aidha, katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)
DSC_9314
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango vyake..
DSC_9331 DSC_9332Kituo cha Afya kilichopo kwa sasa kikiendelea na huduma
Hospitsal
Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilikaMAMCMuonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa
DSC_9350Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akivikwa skafu maalum wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kilumba katika sherehe za kufunga Jubilee ya miaka 50 ya kanisa hilo Jijini Mwanza.
Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi
702
Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50
DSC_9378
Vikundi vya matembezi yakiendelea
DSC_9365 DSC_9368
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo
DSC_9383
Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao.
DSC_9389Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao.
DSC_9398Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride hilo
DSC_9422Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
DSC_9405 DSC_9440 DSC_9443
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo
DSC_9450
DSC_9468Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akitoa salamu katika tukio hilo
DSC_9462
Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hiloDSC_9488Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea vitabu kama kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo vyenye mafunzo mbalimbali
DSC_9500Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ateta jambo na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman ambaye ni Mzee wa kanisa hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Mwanza).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.