ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 19, 2016

DC RORY ATAKIWA KUWATUMBUA WATUMISHI MCHWA WANAOTAFUNA FEDHA ZA HALMASHAURI.


KUTOKA JIMBONI RORYA MKOA WA MARA.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya imemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo, Simon Chacha, kuwatumbua wataalamu watatu wa Halmashauri ya Rorya mkoani Mara waliogeuka mchwa wa kutafuna fedha za mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani pamoja na kudaiwa kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo na kusababishwa kutekelezwa chini ya kiwango.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Samwel Kiboye, kwenye kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichohudhuliwa na DC Chacha ambapo alitambulishwa kwa wajumbe tangu alipoteuliwa na Rais Dk John Magufuli na kuapishwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa,  akitakiwa kusimamia amani, usalama, shughuli za maendeleo na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma..

Kiboye alimtaka DC Chacha, kuanza na Mkuu wa Idara ya Mapato, Afisa Mapato na Msaidizi na Mhandisi wa barabara na majengo wa Halmashauri hiyo ambao wamekuwa wakimzunguka Mkurugenzi na kuwa vinara wa kutafuna fedha za mapato na kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo  kwa kuzingatia BQ (thamani ya fedha) na kuisababishia Halmashauri pia kuwa na matumizi  makubwa yasiyoendana na makusanyo.

“DC tunaomba uiokoe Halmashauri ya Rorya kuna mchwa wa watumishi ambao wamekuwa wakitafuna fedha, tunakuomba uanze na wafuatao Afisa Mapato Mkuu (Martin Kanyambo) na Msaidizi wake (Bahati Lwoga) wasimamishwe na uchunguzi ufanyike wakupe taarifa sahihi kwa nini mapato ya Halmashauri kuanzia Julai 2015 hadi April 2016 yalishuka kutoka Sh milioni 60 kwa mwezi  hadi Sh milioni 16 kabla ya kupanda tena Mei 2016 kufikia Sh milioni 69,”alisema.

Mwenyekiti huyo akiungwa mkono na Mbunge wa Jimbo hilo Lameck Airo (CCM) na  Madiwani wote wa Chama hicho aliposema “DC Chacha chukua hatua za haraka anza na hao lakini pia Mhandishi wa Halmashauri (Mohamed Buberwa) ambaye amshindwa kususimamia miradi ya barabara na majengo ya shule, zahanati na kutekelewa chini ya kiwango lakini Mwekahazina wa Halmashauri (Mwalutamwa) apewe onyo kali na kutojitokeza mapato kushuka ,”alisisitiza.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo, Airo alipopewa nafasi ya kuzungumza aliwataka Madiwani wa Kata 21 kuacha urafiki na wataalamu wenye tabia ya kufuja fedha za mapato ya Halmashauri na badala yake wawe makini kusimamia makusanyo katika vyanzo vya mapato ya ndani vilivyopo kwenye Kata zao ambapo jukumu hilo wamepewa watendaji wa Kata wanaodaiwa kushindwa kutoa risti halali na kile walichokusanya.

“Madiwani wenzangu tunazvyo vyanzo ambavyo ni mialo, magulio na minada lakini watendaji wanaokusanya huwasilisha mapato kiduchu Benki, wamekuwa wakitoa taarifa za uongo hivyo jitokezeni kufatiria na kuomba kupitia vitabu vya risti katika makusanyo ya siku na mwezi kwenye Kata zetu ukiona taarifa ya Februari 2016 tumekusanya mapato kiduchu asilimia 30 tu ili Halmashauri isifutwe na serikali tufikie asilimia 80 ya lengo,” alisisitiza.

Kwa upande wake DC Chacha ameuhakikishia uongozi wa CCM Wilaya, Mbunge Airo na wajumbe wa kikao hicho kufatiria na kuwachukulia hatua kwa watendaji na watumishi watakaobainika kusababisha kushuka kwa kasi mapato ya Halmashauri hiyo na waliohusika kutafuna fedha ambapo taarifa  inaonyesha kukusanya Sh milioni 16 badala ya Sh milioni 60 za awali walipokuwepo mawakala na kabla ya baraza la madiwani kuvunjwa Juni 30 mwaka 2015.

“ Rais Dk Magufuli alituagiza kusimamia mapato na matumizi ya fedha kwenye Halmashauri ikiwemo miradi ya maendeleo iendane na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali hivyo niwahakikishie sitokuwa na kigugumizi kuchukua hatua kwa watumishi wezi na wanaomba rushwa wakati wa kutoa huduma kwa wananchi na madiwani acheni kuwatetea watumishi wabovu wanaotafuna fedha,”alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.