ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 18, 2016

BREAKING NEWS: MADAKTARI HOSPITALI YA BUKUMBI WILAYANI MISUNGWI MKOANI MWANZA WAGOMA.

Hali siyo shwari kwa wananchi wanaokwenda hospitali ya Bukumbi wilaya ya Misungwi kupata tiba.

Huduma za afya kwa baadhi ya vitengo muhimu hospitalini hapo zimesimama kufuatia kufuatia mgomo wa watumishi wa Afya na madaktari wa Hospitali hiyo Misheni inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Misungwi.

Kwa mujibu wa baadhi ya madaktari ambao hawakutaka kutaja majina yao mpaka hatua ya majadiliano itakapo malizika wamesema yapata mwezi sasa watumishi wa hospitali hiyo hawajapata mishahara na stahiki zao.

Siku ya Ijumaa watumishi hao waliuandikia barua uongozi kwamba ikifika Jumatatu hawajapata mishahara yao hawataingia kazini ila watafanya kazi.

Leo asubuhi na mpaka sasa uongozi umekuwa ukihangaika huku na kule kuwasihi wauguzi hao kurudi kazini kawaida wakati mambo yakiwekwaa sawa, lakini mpaka tunapenyeza taarifa hizi mambo si shwari na vikao vinaendelea.

Inasemekana Jumla ya wafanyakazi wapatao 100 na ushee wako kwenye mgomo huo ile hali wafanyakazi wengine wasiozidi 25 ambao ni waajiliwa wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi wao wako kazini kwani mishahara yao imeshalipwa na Serikali.

Jembe Fm inaednelea kufuatilia taarifa hii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.