ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 11, 2016

AIRTEL NA VETA YAITAMBULISHA VSOMO KWA MAKUNDI YA VIJANA YA JIJINI ARUSHA.

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Mushashu Anaclet (wa pili kushoto) akiongea wakati wa kutambulisha mpango wa mafunzo ya VSOMO kwa kiongozi wa Bodaboda Kelvin Adam kuashiria uzinduzi wa masomo ya ufundi kwanjia ya simu za mkononi yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na VETA
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Mushashu Anaclet (wa pili kushoto)akitambulisha mpango wa mafunzo ya VSOMO kwa kiongozi wa Bodaboda Kelvin Adam kuashiria uzinduzi wa masomo ya ufundi kwanjia ya simu za mkononi yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na VETA
baadhi ya wakazi wa mkoa wa Arusha wakipokea vipeperushi vyenye maelezo ya VSOMO
Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba akitoa maelezo ya VSOMO kwa vijana mkoa wa Arusha
baadhi ya wateja wakijiunga na mtandao wa Airtel ili kupata mafunzo ya VETA kwa njia ya simu zao za mkonono maarufu kama VSOMO

 Airtel na VETA yaitambulisha VSOMO kwa makundi ya vijana jijini Arusha
Airtel kwa kushirikiana na VETA mwishoni mwa wiki imewafikia vijana mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, madereva wa bodaboda katika mkoa wa Arusha na kuwahamasisha kujiunga na masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu za mkononi ili kukabiliana na tatizo la ujuzi linalosababisha wengi kukosa ajira
Masomo hayo kwa njia ya mtandao ya VSOMO yatawapatia vijana mwanya wa kuongeza ujuzi ambapo kwa sasa kozi 5 zinapatikana hivyo mteja wa Airtel ataweza kuchagua masomo anayotaka kusoma na kisha kupatiwa vyeti vinavyotambulika katika soko la ajira.
Baadhi ya wajasiriamali na madereva bodaboda wa kituo cha MOUNT MERU jijini ARUSHA, wamesema hatua hiyo ni nzuri kwani itawapa fursa yakujiendeleza.
Akiambatana na Airtel pamoja na VETA, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Mushashu Anaclet  aliongelea mpango huu na kusema” hatua hiyo itatoa fursa kwa watu wengi kupata elimu kwa muda muafa ambayo itakuwa nguzo katika maisha yao ya kila siku. Tunawapongeza Airtel na VETA kwa kuanzia mpango huu ambao utachochea kuwa na jamii wenye ueledi, ujuzi na elimu ya kutosha na kuchochea kukua kwa uchumi.
Meneja wa mradi huo, toka VETA, Mhandisi  Lucius Lutenganya  amesema mpango huo utaongeza wigo mpana kwa vijana wengi kuweza kusoma kwani tumekuwa tukipokea maombi maeneo mengi kila mwaka

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.