ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 9, 2016

20% adai ujio wake mpya unawafanya wasanii wengine watamani kujificha.Msanii wa muziki aliyewai kutamba na wimbo ‘Malumbano’ 20% amedai baada ya kurudi chini ya Label ya ‘Combination Sound’ chini ya producer Man Water, kuna wasanii ambao hawajapenda.


Muimbaji huyo ambaye alishinda tuzo tano za Kilimanjaro Music Award mwaka 2011, amesema kuwa, kurudi kwake Combination Sound kuna wasanii wanaona watakosa nafasi zao katika muziki.

“Nikwambie tu kuna mwanamuziki ambaye hana uwezo wa kuandika mashairi kama 20% hawezi kufurahia muungano kati yangu na Man Water kwa sababu anajua tayari balaa limeshaanza, vumbi linakuja, kwa hiyo huyo huyo msanii alikuwa ana support ugomvi kati ya 20% na Man Water,” alisema 20%

Pia muimbaji huyo alisema tuzo za Kili ndio kitu ambacho kimchanganya na kumfanya apotee kwenye game.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.