ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 21, 2016

WAFANYAKAZI KIWANDA CHA MWATEX WASHINDA KESI DHIDI YA SERIKALI.

Hatimaye wananchi waliowahi kuwa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo MWATEX cha jijini Mwanza wameshinda kesi ya kudai stahiki zao.

Kesi hiyo ya mwaka 1995, ilifunguliwa na wafanyakazi hao mnamo mwaka huo baada ya kiwanda hicho kudaiwa kufirisika na kuwaondoa wafanyakazi hao pasipo kuwapa barua za kuachishwa kazi.

Baadhi ya wafanyakazi hao walio wahi kuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho, wamesema licha ya kuwa wameshinda kesi lakini hukumu hiyo haijaeleza wazi juu ya stahiki zao kwamba ni kiwango gani wanatakiwa kulipwa licha ya kukaa bila malipo kwa zaidi ya mika kumi na tano.

Zaidi ya wafanyakazi 1700 wanasubiri kuona nini Serikali itafanya juu ya stahiki zao kupitia hukumu iliyotolewa mnamo tarehe 14 mwezi huu.

Rozaria Lymo ni mmoja kati ya wafanyakazi waathirika wa kiwanda hicho walio zungumza nasi, akisema amekuwa mfanyakazi wa kiwanda hicho tangu mwaka 1972, akitaja kuwa bado bado hawajajua nini mstakbar wa malipo yao, kwani kuna fufunu zinazo dai kuwa watalipwa kwa viwango vya mishahara ya zamami ile hali kadri miaka ikisonga mbele viwango hata vile vya kima cha chini cha mshahara vimekuwa vikibadilika sembuse wao.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA WALICHOSEMA.
Baadhi ya wafanyakazi wametoa ushuhuda kuwa kuna baadhi ya watendakazi wenzao ambao wamepoteza maisha kutokana na mfadhaiko na msongo wa mawazo, familia zimeharibika kwa watoto kushindwa kwenda shule, ndoa zimevunjika kwa kukosa kipato huku wengine wakipata maradhi ya ajabu kutokana na msongo wa mawazo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.