ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 11, 2016

KERI HILSON ATUA NCHINI NIGERIA KWA FINALI ZA MASHINDANO AIRTEL TRACE MUSIC STARS AFRIKA (2)

Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Afrika, Dia Ezzaoudi
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Lagos nchini Nigeria. 
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha  pamoja na Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga
Wafanyakazi wa Airtel kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha pamoja na Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari. Pichani (wa pili kushot) Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania , Bi Jane Matinde

Mwanamuziki nguli nchini Marekani, Keri Hilson ameingi nchini Nigeria ili kushiriki  katika shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika linaloshiriksha nchi 9 barani Afrika ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanadada Melisa John.

Keri Hilson atashirikiana pamoja na majaji wengine katika kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika kwa mwaka 2016. Ambapo Taji la ushindi wa Airtel Trace Music Stars 2015 linashikiriwa na Nalimi Mayunga kutoka Tanzania

Siku moja baada ya kuwasili , Keri Hilson ameshiriki katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alihainisha kuvutiwa kwake na washiriki na kukiri kwamba bara la Afrika lina  vipaji vingi vya muziki na kuwapongeza Airtel na Trace kwa kuanzisha mpango huu wenye lengo la kuinua vipaji na kuwawezesha vijana kuvifikia ndoto zao

“ naamini finali itakuwa na mvuto sana nimekutana na washiriki  na kushuhudia vipaji vya kutosha.  Mambo makuu tutakayoangali wakati wa  fainali ni pamoja na  uwezo wa mshiriki kuweza kutoa burdani , uwezo wa sauti yake na jinsi gani anaweza kutoa burdani kwa mashabiki. Naamini mashindano ya kesho yatakuwa na mvuto nanimejiandaa vyema kufanya kazi na mshiriki atakayeshinda kwa mwaka huu”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.