ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 19, 2016

HAPPY FATHER'S DAY

Japo leo ni siku ya wanaume duniani, kuko kimyaaaaa na sijasikia cho chote kwenye redio na vyombo vingine vya habari mapema kuhusu siku hii muhimu. 

Lakini mbona siku ya wanawake tunasikia matayarisho, tena wiki kadhaa kabla kuelekea siku husika na ikifika siku husika ndiyo penyewe hapa utasikia matamko na keleke zikipazwa kila kona hadi mitandaoni.

Mbona siku yetu akina baba tunaidharau namna hii? Au kwa vile ni sikukuu iliyoanza hivi karibuni tu (2009)? Au ni kwa vile hatuna mchango muhimu katika jamii mbali na kuanzisha migogoro na vita, kuendeleza mifumo dume yenye kunyanyasa akina mama na masaibu mengineyo? 

Mmmh inabidi kujitathimini......Jeh tuna muda kuhusu hilo.

Mwaka 2010 sikukuu hii iliadhimishwa kwa mara nyingine hapa nchini Tanzania kwa kuanzishwa rasmi Chama Cha Wanaume Wanaopigwa Tanzania (CCWWT) na baadhi ya kanuni za chama hiki zinapatikana mitandaoni (MUDA MCHACHE NAKUPA ANUANI HAPA).

Hongereni wanaume popote mlipo hapa duniani; na hasa akina baba mnaoshiriki kikamilifu katika malezi ya watoto.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.