ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 14, 2016

AIRTEL NA FACEBOOK WAZINDUA "BILA SALIO WALA MB KAMPENI"

Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty akizungumza  kwenye uzinduzi wa kampeni ya  “Bila Salio Wala MB” iliyozinduliwa jana katika hafla iliyofanyika ofisi za makao  makuu ya Airtel, ambapo wateja  wa Airtel wanapata huduma ya Facebook, Messenger na huduma nyingine zinazopatikana kwenye facebook bure kabisa.
Airtel na Facebook wazindua “Bila Salio Wala MB kampeni”

• Unapata Facebook na messenger bure kabisa
• Wateja wa Airtel wanapa huduma hizi bure  bila ya kuwa na muda wa maongezi  au intaneti
• Huduma hii Inapatikana kwa wateja wote wa Airtel

Dar Es Salaam, 14 Juni 2016 Airtel Tanzania, kwa kushirikiana na Facebook, imezindua huduma ya  Bure  ya Facebook kwa wateja wa Airtel katika kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la  "Bila Salio Wala MB". 

Lengo la mpango huu ni kuunganisha kila Mtanzania katika intaneti  na, kwa njia hii, kutawezesha kufungua fursa nyingi ambazo hapo awali zimekuwa ngumu kwao kuzitimiza.

 Kama sehemu ya "Bila Salio Wala MB" kampeni, Watanzania wenye kadi ya simu ya Airtel na simu yenye uwezo wa kupokea intaneti wataweza kufurahia Facebook, Messenger na huduma nyingine zinazopatikana kwenye facebook.

 Ndani ya Facebook, wateja wataweza kuchat, kutuma picha, video , kutoa maoni, kuweka picha, kuangalia picha na mambo mengine mengi.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty alisema, "kutokana na maisha ya sasa jinsi yalivyo intaneti ni kitu muhimu sana katika maisha ya watu kwani imekuwa ikileta maendeleo katika Jamii na uchumi duniani kote. 

Lengo letu ni kuunganisha watu wengi itakavyowezekana na intaneti  na kuwatambulisha katika fursa mbalimbali zilizopo kwa kukuza uchumi wao . Tunaamini kabisa huduma hizi za bure za facebook ni hatua ya kwanza nzuri ya kufikia lengo hili. "

  Free Basics ni seti ya Kiswahili  na tovuti ya kimataifa Tanzania inayotoa Habari za  afya, elimu, biashara na habari za  fedha husiana na watu ili waweze kufanya uamuzi na maamuzi ya kuboresha maisha yao.  

Free Basics   ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii duniani kote , inayowawezesha wateja kuwasiliana kwa urahisi na ndugu jamaa na marafiki zao. 

Kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata huduma hii  bila gharama yoyote  , inatoa fursa kubwa kwa mamilioni ya watu , urahisi zaidi wa kuwasiliana na pia kuweza kutangaza bidhaa mbali mbali na hivyo kuweza kujiongezea kipato huku wakitumia mtandao huo wa facebook kwa kibiashara zaidi ya mawasiliano pekee na kukuza uwezo wao kutokana na utajiri wa habari wanazoweza kupata kupitia mtandao.

  Akitoa maelezo, mkuu wa kitengo cha intaneti Gaurav Dhingra alielezea "utumiaji wake ni rahisi. Popote ulipo Tanzania, ilimradi unakadi ya simu ya Airtel iliyosajiliwa  katika simu yako yenye uwezo wa kupata intaneti , unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook, na kufurahia kabisa, huduma hiyo bila ya kuwa na salio au kifurushi cha intaneti. 

Kwa wale ambao sio watumiaji wa Facebook wanaweza pia kuomba njia fupi ya kuunda akaunti zao kwa kupiga *148*88 #, "aliongeza Dhingra.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.