ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 19, 2016

WATATU WAUAWA NA MAPANGA MWANZA WAKIWA MSIKITINI AKIWEMO SHEIKH

Watu watatu wameuawa kwa kukatwa mapanga na mashoka na mwingine mmoja kujeruhiwa kichwani wakati wakifanya ibada katika msikiti wa Masjid Rahmani uliopo eneo la Ibanda Relini wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Kwamujibu wa habari za kiuchunguzi zinasema kuwa watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga, shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla katika msikiti wa Rahmani na kuwakuta waumini wakiswali na kuzima taa na kutoa sauti wakisema "Kwanini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiliwa na Polisi?" kisha hapo hapo wakaanza kuwakata kwa mapanga baadhi ya waumini katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Walipata majereha makubwa sehuemu mbalimbali za miili yao, shingoni, kichwani, mikononi na walipoteza maisha wakati wakikimbizwa hospitali ya wilaya ya Nyamagana Butimba.

Waliouawa ni Feruz  Ismail Elias (27) kabila Muha imamu wa msikiti huo na mkazi wa Ibanda Relini, Mbwana Rajab (40) kabila Mbondei mfanyabiashara na mkazi wa Ibanda, Khamisi Mponda (28) dereva wa kiwanda cha samaki cha (TPF) mkazi wa Mkolani, wote walijeruhiwa sehemu za kichwani, shingoni na mikononi.

Aliyejeruhiwa ni Ismail Abeid Ghati (13) Mkurya mwanafunzi wa madrasa katika shule ya kiislamu iitwayo Jabar Hila iliyoko maeneo ya Nyasaka ambaye huyu alipata majereha kichwani na anapata matibabu katika Hositali ya Nyamagana.

Kutokana na hali hiyo waumini wengine  walifanikiwa kukimbia huku wakipiga mayowe yaliyopelekea wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti chupa mbili za vilevi zilizokuwa na petroli na tambi za moto ambapo chupa moja ililipuka lakini haikuleta madhara makubwa.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watatu wanaodhaniwa kuhusika na tukio hilo, huku msako mkali ukiendelea kuwasaka wengine waliohusika kwa namna moja au nyingine kwenye mauaji hayo.

"Napenda kuwasihi wananchi watulie wakati huu tukiendelea kufanya upelelezi, pia natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapohisi mazingira ya shaka yenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kiuhalifu yasiyo ya kawaida ndani ya himaya zao au nje ya maeneo yao" alisema Kamanda Msangi.

Aidha kamanda ametoa ushauri kwa wananchi nyumba kwa nyumba (mabalozi), nyumba za ibada, pamoja na wamiliki wa kumbi za starehe kusisitiza ulinzi shirikishi kwa hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.