ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 19, 2016

TFDA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA WADAU KUHUSU USALAMA WA CHAKULA BARANI AFRIKA



Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, akitoa maelezo ya awali katika ufunguzi wa mafunzo kwa washiriki wa Kongamano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Bara la Afrika. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya siku tano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Afrika. Wengine waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Bi. Charys Ugullum, Mwakilishi wa FAO na Mwakilishi wa IAEA, Bw. Alex Mulori. 

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa mwenyeji wa mafunzo ya siku tano, tarehe 16 – 20 Mei, 2016, kwa wadau wa udhibiti katika mnyororo wa Usalama wa Chakula hususan upimaji katika maabara Barani Afrika.
 
Akifungua mafunzo hayo yaliyowashirikisha wadau wapatao 50 kutoka nchi 15 za Afrika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, alisema kuwa Lengo kuu la mafunzo na mkutano ni kujadili majukumu, wajibu na mchango wa kila mdau katika suala zima la kuhakikisha chakula ni salama kwa walaji. 

Dr. Mpoki alisema, “ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa wa namna bora ya usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa Chakula Salama kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau mliopo hapa’ . 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, wakati wa kutoa maelezo ya awali kuhusu mafunzo hayo yanayodhaminiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Nguvu za mionzi (IAEA), alieleza kuwa kufanyika kwa mafunzo haya nchini Tanzania ni heshima kubwa na ishara ya mwendelezo wa TFDA kufikia Dira yake ya kuwa taasisi inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa Tiba. 

Nchi zinazoshiriki katika mafunzo haya ni pamoja na Algeria, Benin, Botswana, Cameroon, Egypt, Ethiopia, Mauritius, Mali, Chadi, Namibia, Sudan, Tunisia, Uganda, Zimbabwe na Tanzania. Matokeo ya mafunzo haya yatakuwa ni dira ya utekelezaji wa mradi wa udhibiti wa mnyororo wa Usalama wa Chakula kabla ya kufikia mwisho wa mwezi Disemba 2016. 

Wadau wa mnyororo wa udhibiti wa Usalama wa Chakula walioshiriki katika mafunzo haya wanatoka kwenye maeneo ya maabara, ukaguzi, uzalishaji wa vyakula na walaji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.