ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 3, 2016

RUNGU LA TFF LAPELEKA VILIO VIONGOZI NA VILABU.


Kamati ya rufaa ya nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini TFF zimetupilia mbali rufaa za warufani saba kati ya nane zilizokatwa juu ya sakata la upangaji wa matokeo katika michezo ya mwisho ligi daraja la kwanza.

Wakili Revokatusi Kuuli amesema, rufaa ilikuwa na warufani nane ambao ni Timu ya Geita Gold, Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC, Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold, Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora, Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma, Timu ya Soka ya Polisi Tabora, JKT Oljoro Fc ya Arusha na Yusufu Kitumbo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora.

Wakili Kuuli amesema, kutokana na ushahidi uyliopelekwa na ukasikilizwa, watumhumiwa saba wote wamekutwa na hatia na bado wataendelea na adhabu huku Mlinda mlango wa Geita Gold Denis Richard Dioniz amefutiwa hatia kutokana na utetezi uliopelekwa na ataendelea na masuala ya soka.


Wakili Kuuli amesema, warufani wote wamepewa haki ya kufanya marejeo ndani ya muda unaotakiwa kisheria kuanzia leo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.