ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 10, 2016

MENO YA TEMBO YAKAMATWA NDANI YA KANISA, MCHUNGAJI NA WATUMISHI 4 WAHUSISHWA

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu watano akiwemo Mchungaji wa Kanisa la Moravian kijiji cha Usevya kwa kukutwa na nyara za serikali vikiwemo vipande kumi na moja (11) vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo ishirini nukta tatu (20.3) walivyokuwa wamehifadhi katika mfuko wa sandarusi na kufichwa ndani ya kanisa hilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa katavi Damas Nyanda amesema tarehe 5/5/2016 majira ya saa nane na nusu mchana huko katika kata ya Usevya wilaya ya mlele Polisi walikamata pembe hizo za ndovu zenye thamani ya shilingi milioni tisini ndani ya ofisi ya Kanisa la Moravian huko katika kijiji cha usevya.

Kamanda huyo ameongeza kuwa msako wa kuwakamata wahalifu uliendelea ambapo tarehe 8/5/2016 majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha Mgolokani kata ya Stalike polisi ilimkamata mtu mmoja akiwa na jino moja la tembo na nyama ya nyati kilo moja, ambapo pia siku hiyohiyo katika kitongoji hicho majira ya saa tatu na nusu asubuhi polisi walimkamata mtu mmoja akiwa na jino la simba baada ya kufanya msako nyumbani kwake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.