ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 9, 2016

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LIMEKAMATA BUNDUKI MOJA NA RISASI 144.

JESHI la polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kijihusisha na kikundi kinachowapora watoa huduma za fedha kwa njia ya mtandao (M-PESA) mkoani Mwanza. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema watu hao wamekamatwa katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Bugarika Jijini Mwanza na kufanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG, Kofia za kufunika uso pamoja na makoti.


KAMANDA MSANGI amesema bado wanaendelea na jitihada za kukisambaratisha kikundi hicho ambacho kinadaiwa kusababisha mauaji ya wafanyabiashara wa mihamala ya fedha na wengine kuwasababishia majeraha ya kudumu na ulemevu wa maisha.


Kamanda Mohamed Msangi, Kamishna mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza amesema kuwa bado jeshi lake linaendelea kuwasaka majambazi wengine. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.