ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 8, 2016

VIGOGO CHADEMA KYELA WAVULIWA UONGOZI KWA USALITI.

Kyela. 
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Saadati Mwambungu pamoja na  wajumbe 19 wa Kamati ya Utendaji wa wilaya hiyo wamevuliwa uongozi baada ya kutuhumiwa kukihujumu chama hicho.

Hatua hiyo ilifikiwa juzi jioni na uongozi wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, chini ya mwenyekiti wake, Dk Stephen Kimondo, Mratibu wa Kanda, Frank Mwaisumbe na kuweka wilaya hiyo chini ya uangalizi wa uongozi wa Mkoa wa Mbeya ndani ya 30 wakati wakiendelea na uchunguzi.

 Mratibu wa Chadema Kanda hiyo, Frank Mwaisumbe aliliambia gazeti hili jana kwamba baada ya kufanyia kazi tuhuma 17 zilizowasilishwa kwao na wanachama wa chama hicho wilaya , walibaini kuwa tuhuma saba kati yake zina ukweli dhidi ya viongozi hao hivyo wakafikia uamuzi wa kuwasimamisha na kuwataka kurudisha mali zote za chama hicho ndani ya siku 30.

 Mwambungu alipoulizwa juu ya kutimuliwa kwao, alikiri huku akisisitiza kwamba tuhuma zilizotolewa dhidi yao hazina ukweli wowote kikatiba bali zimetengenezwa na ‘genge’ la watu wachache kwa uchu wa madaraka.

Hata hivyo, alisema hana kinyongo kusimamishwa uongozi kwa kuwa suala hilo lipo kikatiba ndani ya chama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.