ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 17, 2016

MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM NA BAGAMOYO KUKOSA MAJI KWA SAA 10




TAARIFA KWA UMMA
                                                                        17/5/2016
KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU CHINI
Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam  pamoja na  Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 10 kuanzia saa 5 asubuhi Jumanne, Tarehe 17/05/2016.
Sababu za kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Chini ni kuzuia uvujaji uliotokea mtamboni kwenye bomba la inchi 72.
Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es salaam kukosa Maji:
MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

Maeneo Mengine ni

MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO-MAKAO MAKUU

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.