ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 31, 2016

TBL YAIBUKA MSHINDI


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo  kwa mshindi  wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015, kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  wakati wa hafla ya kutoa  tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia)  na kushoto ni Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo


TBL Group yaibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya mzalishaji bora wa mwaka 2015

Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.

Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI nahafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.

Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.

“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.

Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.

“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.