ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 27, 2016

MKUTANO WA MAKONDA NA WASANII ALHAMISI HII.

WANAMUZIKI NA WADAU WA MUZIKI KUKUTANA NA MKUU WA MKOA DSM ALHAMISI HII

Wanamuziki wa dansi, taarab, bongo fleva na wadau wa muziki waishio Dar es Salaam, Alhamisi hii watakutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ili kubadilisha mawazo juu mwenendo wa kazi zao.

Wasanii na wadau hao watakutana na Makonda ndani ya ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kuanzia saa 5asubuhikatika mkutano utakaohudhuriwa pia na wamiliki wa kumbi za starehe wa mkoa wa Dar es Salaam.

Mkutano huo umeandaliwa na kamati ya ushirikiano ya wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za starehe iliyoundwa hivi karibuni ili kujadili kwa undani changamoto za sheria ya biashara ya vileo na burudani ambazo ziko tangu mwaka 1968 na 1972.

Mmoja wa wasemaji wa umoja huo wa wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za starehe, Juma Mbizo, ameuambia mtandao huu kuwa maombi yao ya kumwalika Mkuu wa Mkoa katika mkutano huo, yameshawasilishwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa.

Jumba Mbizo amewataka wanamuziki, wadau wa muziki na wamiliki wa kumbi za starehe watakaopata taarifa za mkutano huo kwa njia yoyote ile, wafike kwa wingi Vijana Social.


Mbizo amesema mkutano huohauhusiani na chama chochote cha muziki, bali umeandaliwa na waathirika wakuu sheria hizo za burudani na vileo ambao ni wanamuziki na wamiliki wa kumbi za starehe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.