ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 26, 2016

MADAKTARI WA UPASUAJI MUHIMBILI WAWEKA KAMBI MWANZA KUWAFANYIA UPASUAJI BURE WATOTO WENYE KICHWA KIKUBWA NA TATIZO LA MGONGO WAZI.

Halphan Kiwamba ni Afisa Habari wa Kampuni ya GSM Foundation (kulia) akiwa na daktari Bingwa wa Ubongo, mgongo na Mishipa ya fahamu Dr. Othman  W. Kiloloma kutoka Hospitali ya Taifa ya Rufaa Muhimbili katika mahojiano na kipindi cha KAZI NA NGOMA kinachorushwa na kituo cha radio Jembe Fm Mwanza.
Wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 27 hadi 30 katika hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza kuwaleta watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi, Matibabu yote hayo ya upasuaji yakifanywa bure kabisa kwa wazazi wote wanaoishi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma na Morogoro. 
Daktari Bingwa wa Ubongo,mgongo na Mishipa ya fahamu Dr. Othman  W. Kiloloma kutoka Hospitali ya Taifa ya Rufaa Muhimbili akifafanua jambo katika mahojiano na kipindi cha KAZI NA NGOMA kinachorushwa na kituo cha radio Jembe Fm Mwanza.
Tiba hii ikiwa imefadhiliwa na GSM Foundation imetaja uwepo wa Madaktari bingwa wa upasuaji wa kichwa kikubwa na mgongo wazi, kutoka taasisi ya mifupa (MOI) ambao ndio watakao simamia zoezi hilo.
Nchini Tanzania, Jumla ya watoto 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila Mwaka. kati yao ni watoto mia nne tu wanaorudi hospitalini kwaajili ya matibabu ambayo mara nyingi uwa ni upasuaji. 

Madaktari waliopo Tanzania wanaoweza kufanya operesheni hizi wako 9 tu. 

Mmoja anapatikana Mwanza Bugando na nane wanapatikana Dar es salaa.

Kufuatia changamoto hiyo Taasisi ya GSM kwa kushirikiana na kitengo cha upasuaji wa mifupa MOI wameandaa kambi za TIBA katika mikoa yote ya Tanzania.

Wataanzia Mwanza kisha Shinyanga, halafu Singida, Dodoma na kumalizia Morogoro. Kujua ratiba na tarehe ya mkoa wako sikiliza na fuatilia vyombo vya habari vilivyopo karibu nawe.
Afisa Mahusiano wa Taasisi ya Sayansi ya Jamii Tanzania Bw. Bituro Kaizeri akishiriki zoezi la ubandikaji wa matangazo ya huduma ya Afya bure kwa upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi Mwanza, zoezi linaloanza wiki hii tarehe 27 hadi 30 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando. BOFYA PLAY KUSIKILIZA ALICHOSEMA.

Mwanahabari Peter Fabian wa gazeti la Mtanzania naye kashiriki nasi.
Halphan Kiwamba ni Afisa Habari wa Kampuni ya GSM Foundation hapa anazungumza na Jembe FM. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
"Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako" Mwanahabari kutoka Jembe Fm Mwanza Albert G. Sengo, kaivalia njuga kampeni hii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.