ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 23, 2016

LIGI KUU UINGEREZA LIVERPOOL PASU KWA PASU NA NEWCASTLE, MANCHESTER CITY YAPAA HADI NAFASI YA TATU.


Manchester City imepanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Stoke City 4-0 huku ikitarajiwa kumenyana ana Real Madrid katika kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.

Fernando alifunga kwa kichwa na kuwaweka City kifua mbele kabla ya Sergio Aguerro kufunga kwa njia ya Penalti.
Baadaye Kelechi Ihienacho aliyetangazwa mchezaji bora katika mechi hiyo alifunga mabao mawili.
Eden Hazard alifunga bao lake la kwanza na kuisadia timu yake kuishinda Bournemouth.
Cesc Fabregas alisaidia katika mabao matatu ya Chelsea akitoa pasi nzuri kwa wafungaji Pedro,Hazard na baadaye Willian.
Vilevile Newcastle iliimarisha matumaini yao ya kusalia katika ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare ya 2-2 na wenyeji Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Daniel Sturridge na Adam Lalana waliiweka mbele Liverpool kabla ya Newcastle kukomboa kupitia Papis Cisse na Colback .

Liverpool vs Newcastle 2 2 All Goals & Highlights Premier League 23/4/2016

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.