ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 27, 2016

WANARIADHA ALA SABUNI WAKIDHANI NI CHAKULA.

CHANZO BBC SWAHILI.

Wanariadha waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijipata wamekula sabuni baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa lugha ya kiingereza.

Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily.
Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinuka harufu nzuri .
Walioshuhudia wanasema kuwa sabuni nyingi zilitupwa kandakando ya barabara huku zikiwa zimeumwa.
Tatizo ni kwamba sabuni hizo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na hivyobasi wanariadha hao hawakuelewa lugha hiyo kulingana na gazeti hilo.
Hatahivyo walioandaa mbio hizo waliomba msamaha.Pakiti za sabuni hizo zilikuwa kama zile za chakula.
Sabuni zilizowekwa katika pakiti na kunukia vizuri kamachakula.
Pia kulikuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya majeraha katika mbio hizo huku wanariadha 12,200 wakihitaji kupatiwa matibabu wakati na hata baada ya mbio hizo.
Haijulikani ni majereha mangapi yalisababishwa na kisa hicho cha sabuni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.