ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 23, 2016

WANANCHI WA WILAYA MPYA YA KIBITI WAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA NISHATI YA UMEME

Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando kulia akiwa na mwandishi wa habari hizi Victor Masangu mara baada ya kufanya mahojiano kuhusiana na changamoto zinazowakabili wananchi wake  pamoja na mikakati aliyojiwekea  baada ya Kibiti kupandishwa adhi kuwa Wilaya mpya.

NA VICTOR MASANGU, RUFIJI    

WANANCHI wa Wilaya mpya ya Kibiti Mkoani Pwani  kwa sasa wanakabiliwa na  tatizo kubwa la upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme, kwa kipindi cha muda mrefu jambo ambalo linakwamisha kwa kiasi kikubwa katika  kuendesha shughuli zao za  kimaendeleo.

Wakizungumza na  kwa nyakati tofauti  katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando kwa ajili ya kuweza kutoa shukrani kwa kuchaguliwa kushika anafasi hiyo  pamoja na  kuweza kubaini changamoto mbali bali  zinazowakabili wananchi wake ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Wananchi hao akiwemo  Nuruel Moshi pamoja na Mohamed Ngogota   walisema kwamba licha ya Kibiti kupandishwa adhi ya kuwa Wilaya lakini hali ya kiuchumi inazidi kuwa mbaya kutokana na watu wengine katika eneo hilo  wanaendesha maisha yao kwa kutegemea nishati ya umeme  hivyo.

Waliongeza kuwa kwa kipindi hiki  wamejikuta wanashindwa kutimiza malengo waliyojiwekea kwani  bidhaa  zao  nyingi  kwa sasa zimeharibika  ikiwemo samaki nyama, na maziwa, juice pamoja na mambo mengine kutokana na kukosa nishati hiyo ya umeme hivyo wameiomba serikali kulitafutia ufumbizi wa haraka suaa hilo .

Nao wakinamama ambao wanajishughulisha na biashara za kuuza chakula mbali mbali  akiwemo Zawadi Mtunguja  ambaye yeye ni muuguzi katika kituo cha afya Kibiti pamoja Judidhi Mlungu   walisema kwa kutokuwepi kwa umeme kwa upande wao kumewaathiri  kwa kisi kikubwa kwani biashara zao nyingine hazifanyiki hvyo wanapata hasara.

Kwa upande wake  Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando amewahakikishia wananchi wake kulishughulikia  kwa hali na mali suala hio la umeme na tayari ameshalipeleka kwa uongozi wa  mamlaka husisika na watalifanyika kazi na kuwataka wavute subira.

Wananchi wangu natambua kuwepo kwa chanagmoto hii ya umeme na inawaumiza sana lakini kwa upande wangu nitajitahidi kuisimamia hili suala ili umeme uweze kuwa wa akika kwani natambau wananchi wa jimbo langu la kibiti wanafanya shughuli zao mbali mbai kwa kutegemea nishati hii ya umeme hivyo nitaifanyika kazi kwani nimeshalifikisha kwa viongozi wananaohusika,”alisema Ungando.

Aidha Mbunge huyo alibainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati  kabambe ya kuwasaidia wananchi wake katika kujishughulisha  katika shughuli mbali mbali za kuleta maendeleo hivyo kuwaomba madiwani na viongozi kushirikiana bega kwa bega ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika jimbo hilo.
 
HIVI karibuni Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe  Magufuli alitangaza kuipandisha adhi Wilaya hiyo mpya ya Kibiti ambayo hata hivyo bado inaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi katika sekta  mbali mbali  hivyo kupelekea wananchi wake  kulalamika kutokana na kushindwa kupata huduma zinazostahili kwa wakati.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.