ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 22, 2016

TAMWA WAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MOJA YA WADAU WA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

DSC_7648
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga akifungua mkutano huo wa siku moja jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) leo Machi 22.2016, wanaendesha mafunzo ya siku moja jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi mkutano uliofunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga ambaye ameitaka jamii kuchukua hatua ikiwemo kuachana na unywaji wa pombe kupita kiasi kwani ni hatari kwa jamii.

Katika mkutano huo, ambao umefadhiliwa na IOGT-NTO-Movement pamoja na wanahabari, unawashirikisha wadau mbalimbali kutoka maeneo ya mradi unaoendeshwa na TAMWA ikiwemo maeneo ya Kata ya Makumbusho, Saranga na Wazo wa kupinga ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji pombe kupita kiasi kwa wanawake na watoto.

Katia mkutano huo TAMWA pamoja na wadau wengine wameweza kuwashirikisha wadau wa madawati ya kijinsia, Viongozi wa dini katika jamii pamoja na viongozi wa Serikali ya mitaa na Kata pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari.

Aidha, mambo mbalimbali yamejadiliwa katika mkutano ambapo imeelezwa kuwa katika Kata ya Saranga na maeneo ya Mbezi matatizo makubwa yanayoripotiwa ni pamoja na masuala ya ubakaji wa watoto na vitendo vya kulawitiwa ambapo asilimia kubwa vimehusishwa na pombe.

DSC_7659
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akifungua mkutano huo kwa kusoma hotuba fupi ya namna ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi.
DSC_7673
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi (Hayupo pichani)
DSC_7650
Washiriki wakiendelea na mkutano huo muda huu.
DSC_7758
Mkutano ukiendelea
DSC_7667
Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo
DSC_7678
Baadhi wanahabari washiriki katika mkutano huo
DSC_7729
Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo
DSC_7679
Baadhi ya washiriki kutoka katika maeneo ya jamii wakiwa katika mkutano huo
DSC_7743
Mratibu wa kituo cha usuluhishi na upatanishi wa dawati la jinsia (CRC), Bi.Gladness Munuo akieleza jambo katika mkutano huo.
DSC_7745
Mada ya utangulizi
DSC_7750
Washiriki hao katika mkutano huo
DSC_7737
DSC_7764
Ofisa wa TAMWA katika dawati la Jamii na Jinsia, Bi. Marcela Lungu akitoa mada namna ya madawati ya kijinsia na namna ya kumpokea mteja na namna ya kulitatua.
DSC_7721
Baadhi ya wakuu wa madawati ya jinsia pamoja na viongozi wa TAMWA
DSC_7688
Mkurugenzi wa TAMWA akisalimiana na wadau washiriki wa mkutano huo ambao ni wawakilishi wa wananchi
DSC_7700
Picha ya pamoja washiriki wa mkutano wa siku moja wa namna ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.