ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 11, 2016

TAASISI YA DORIS MOLLEL KWA KUSHIRIKIANA NA CBA WASAIDIA HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

 Meneja Mahusiano wa Benki ya CBA, Caroline Makatu (wa pili kushoto)  akikabidhi msaada wa vitanda na mashine kumsaidia mtoto anayezaliwa kabla ya muda, kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Delilah Moshi, katika hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka Benki ya CBA wakiwa katika picha ya pamoja wadau waliofanikisha msaada huo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TAASISI ya Doris Mollel Foundation (DMF) kwa kushirikiana na Benki ya  CBA wametoa msaada vitanda viwili na mashine tatu za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati vyenye wa vitu vyenye thamani ya Sh.milioni  mbili  katika Hospitali ya  Rufaa ya Mwananyamala  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam  Mkurugenzi wa DMF,  Doris Mollel, alisema  kwa kutambua umuhimu kwa sababu wanawakumbuka  wanawake wanaojifungua kabla ya wakati na kutoa msaada huo ni kutaka  kuokoa uhai wa watoto hao .

“Kutambua thamani ya watoto njiti tumeona katika kuokoa uhai na kuweza kufikia malengo tumeona ..mashine za kuwasaidia kufikia malengo yao kama walivyo watoto wengine…taasisi itaendelea kutoa mchango kwa jamii,” alisema Doris.

Naye Meneja Mahusiano wa Benki ya CBA ,Caroline Makatu amesema  kuna changamoto nyingi  hospitali ikiwemo na uhaba wa vifaa kwa kutambua hilo wametoa msaada huo  ili kusaidia mama na mtoto.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Delilah Moshi amesema wanashukuru kwa msaada huo uliotolewa na taasisi hizo kwa kutambua uwepo wa wanawake na kuziwezesha hospitali.

Amesema kwa sasa shida kubwa iliyopo kwa sasa ni uhaba wa majengo kutokana na nafasi chache za kuhifadhia watoto njiti kwa sababu idadi ya watoto inaongezeka.

“Kutokana na kuwapo kwa mashine za kuhifadhia watoto njiti idadi ya vifo vya watoto hao imepungua hivyo naiomba serikali kuongeza madaktari wa watoto kwani hadi sasa wapo wawili tu,” amesema Mushi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.