ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 27, 2016

MAJAMBAZI WAUWA NA KUJERUHI WATU JIJINI MWANZA.

Watu wawili mamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi na majambazi jijini Mwanza: 

 Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, SACP Justus Mamugisha, akitoa taarifa kwa wanahabari.
Watu wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali za kifedha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Justus Kamugisha, amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa mbili usiku katika eneo la Bugarika Sokoni, baada ya watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi waliokuwa na bunduki aina ya SMG kuvamia katika duka la mfanyabiashara na mkazi wa eneo hilo aitwae Daniel Marwa (30).

Kamanda Kamugisha amewataja waliouawa kuwa ni Julius Wankaba (30) ambae ni dereva bodaboda, pamoja na mfanyabiashara mmoja mwenye duka katika eneo hilo aliefahamika kwa jina la Mama Yuni (35).

Amewataka waliojeruhiwa kuwa ni Magesa Mungari (38), Simioni Charles (26) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando huku wengine wakiwa ni Mwita Ryoba (30), Frank Willium (19), Saumu Said (20), Masumbuko Kanduru (38) pamoja na Emmanuel Francis ambao wanapata matibabu katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo mmiliki wa duka lililovamiwa, wanasema majambazi hao walipofika eneo la tukio walianza kufyatua risasi ovyo ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo wakiangalia taarifa ya habari na wengine wakinywa kahawa,  na hivyo kusababisha wananchi kutawanyika jambo lililosababisha vifo na majeruhi hao.

Katika tukio hilo, Majambazi hao walifanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni Mbili, Vocha za simu za mitandao mbalimbali zinazokadiliwa kuwa za shilingi Laki Nane pamoja na simu sita za wateja.

Kamanda Kamugisha amesema Jeshi la polisi Mkoani Mwanza limeanzisha msako mkali ili kuwakamata waliohusika na tukio hilo, huku likiahidi zawadi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni Moja kwa yeyote atakaesaidia kufanikiwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.