ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 16, 2016

DK.KIGWANGALLA AWAONYA MADAKTARI NA WAUGUZI WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA


Tazama MO tv, kuona video hiyo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wanataalum wa sekta ya afya kuacha mara moja vitendo vya kupokea na kuomba rushwa kwani endapo watabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Dk. Kigwangalla emesema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kuadhimisha siku ya kinywa na meno duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya tiba ya kinywa na Meno, Muhimbili.

Ambapo amesema kuwa kwa utawala huu wa sasa Serikali ya awamu ya tano ni dhama nyingine na hawatamvumilia mtu.

“Ninaona tu, bado kuna wachache wanaojihusisha na vitendo vya kuomba rushwa hapa na pale. Kwa dhama hizi ukikutwa hatutakuurumia na hatutamuurumia mtu kwa hili. Tunapaswa kuweka maslai mapana kwa wananchi tunaowahudumia kwenye mioyo yetu” alieleza Dk. Kigwangalla.

Maadhimiho hayo kwa mwaka huu yenye kauli mbiu “Afya njema ya kinywa ni afya ya mwili mzima” kilele chake kinatarajiwa kufikia tamati Mkoani Morogoro ambapo kwa siku zote hizi hadi kilele, Madaktari watatembelea shule maalum kadhaa za ikiwemo ya Mtoni Maalum, Sinza Maalum, Buguruni Maalum na zingine za Mkoa wa Shinyanga na Morogoro ambapo pia watafanya uchunguzi na matibabu ya bure katika siku zote hizo.

Awali katika ufunguzi huo, kulitanguliwa na matembezi maalum ya KM 10, yaliyoongozwa na Naibu Waziri Dk. Kigwangalla ilikuhamasisha afya njema ya kinywa na mwili katika mapambano hayo.
DSC_6472Matembezi maalum ya ufunguzi wa siku ya maadhimisho ya kinywa na meno yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yakipita eneo la Maktaba Kuu.
DSC_6499Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) aliyeyaongoza matembezi hayo pamoja na viongozi wengine waandamizi akiweo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Maseru (kushoto) na Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro wakiwasili katika viunga vya Eneo la Chuo cha tiba ya meno Muhimbili baada ya kutembea kwa umbali wa KM 10.
DSC_6512Baadhi ya viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembea kwa umbali mrefu wa KM 10 kama ishara ya kufungua maadhimisho ya siku ya tiba ya meno duniani.
DSC_6606Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akisoma hotuba maalum ya ufunguzi huo.
DSC_6641Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba kwa wananchi na wageni waalikwa katika tukio hilo
DSC_6619Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba hiyo
DSC_6655Mkuu wa Shule ya Kinywa na Meno, DK. Elison Simon akitoa hutuba yake katika tukio hilo
DSC_6745Baadhi ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA) wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi, Dk. Hamisi Kingwangalla wakati wa tukio hilo.
DSC_6755Baadhi ya viongozi waandamizi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. Kilele cha maadhimisho hayo kinatarajia kufanyika Mkoani Morogoro Machi 20.2016, ambapo watatoa huduma bure ya tiba ya kinywa na meno. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.