ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 4, 2016

JIPU SEKTA YA ELIMU:- MKUU WA MKOA WA MWANZA AMEAMURU KUKAMATWA KWA WALIMU 8 WA SHULE YA SEKONDARI MIHAMA KWA KOSA LA KUJIHUSISHA NA MAPENZI NA WASICHANA WA KIKE SHULENI HAPO.

Walimu 8 akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mihama katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kujihusisha kimapenzi na wanafunzi shuleni hapo.

Moja ya athari zinazotajwa kujitokeza na hata kuathiri dira ya elimu kwa waafunzi shuleni hapo ni tukio la mmoja wa wanafunzi wa kike shuleni hapo aliyelazimika kuhama mkondo wa Sayansi na kwenda Art kufuatia manyanyaso aliyokuwa akifanyiwa na mmoja wa walimu hao aliyekuwa akimtaka kimapenzi
Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo kuwataka wakamatwe kutokana na uchunguzi wa awali uliofanywa na hatimaye kubainika kuhusishwa na tuhuma hizo. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Licha ya kutaja majina ya wahusika, Hamis Maulid ambaye ni Afisa Elimu mkoa wa Mwanza aliongeza kwa kusema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo kubaini kuwa walimu hao walitenda kosa hilo. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.


Mmoja wa watuhumiwa Joseph D. Malifedha ambaye ni Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari.
Baadhi ya maafisa wa idara mbalimbali zilizo husishwa kwenye uchunguzi huo kwa umakini wakinukuu baadhi ya vipengele muhimu wakati wa usomaji wa taarifa.
Sehemu ya kusanyiko hili imejumuisha waalimu wa shule hiyo waandishi wa habari pamoja na watumishi wa idara za elimu serikalini ndani ya mkoa wa Mwanza.
Maafisa toka idara ya Elimu, Takukuru, Majeshi, Dawati la Jinsia, Chama cha Walimu na wafanyakazi ni sehemu ya kamati.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (kushoto aliyesimama meza kuu) akitoa maelekezo ya nini kifanyike kwa walimu hao kama hatua ya kwanza mara baada ya kukumbwa na tuhuma hiyo.
Jeshi la polisi liliwakamata mara moja watuhumiwa hao kwaajili ya hatua nyingine za kisheria.
Ufafanuzi toka TUKTA.
Baadhi ya wanafunzi wamehamishwa shuleni hapo mara baada ya kukubwa na kadhia hiyo, lakini jeh ni nini hatma ya wanafunzi walio kumbana na udhalimu huo na hata kuaathirika kisaikolojia? Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ANAFUNGUKA ZAIDI.


Watuhumiwa mikononi mwa polisi.

Watuhumiwa mikononi mwa polisi.
Kikao cha maamuzi kilifanyika hapa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.