ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 3, 2016

UNYANYASAJI, MKE AKATA NYETI ZA MUMEWE KISA CHAKULA.

MWANAUME mmoja mkazi wa Igeregere Bugarika jijini Mwanza amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukatwa uume wake na mwanamke anayedaiwa kuwa alikuwa ni mpenzi wake.

Mwanaume huyo ambaye jina linahifadhiwa ameripotiwa kukumbwa na mkasa huo siku ya juma mosi wiki iliyopita nyumbani kwake.

Baadhi ya majirani wa mwanaume huyo wamesema mwanamke aliyefanya tukio hilo alikuwa amelewa na sababu za ugomvi huo ni chakula. BOFYA PLAY KUSIKILIZA MKASA.


Siku ya tukio mwanaume huyo alifika nyumbani kwake akiwa amechoka akitokea shamabi alikokuwa amekwenda kulima.

Baada ya kufika nyumbani hakumkuta mwanamke huyo ambapo aliamua kupika na kumuachia chakula kidogo mwanamke huyo.

Mwanamke anayetajwa kufanya tukio hilo akiwa amezungukwa na majirani chini ya ulinzi na pembeni ni jembe dogo ambalo alitaka kufanya ukatili zaidi.
Muda mfupi baadaye mwanamke huyo alifika akiwa amelewa na kudai chakula na baada ya kubaii hakikuwa kinatosha ndipo alipoamua kuzua ugomvi uliopelekea kupoteza fahamu kwa mwanaume huyo na kisha mwanamke huyo kupata nafasi ya kumkata uume mwanaume huyo kwa kisu.

Mwenyekiti wa mtaa huo Dankani Nyamgonja amesema matukio ya aina hiyo yanapaswa kukemewa kwa nguvu kubwa kwa kuwa yanaondoa utu.


Jitihada za kuzungumza na jeshi la polisi ili kufahamu hatua zilizochukuliwa hadi hivi sasa bado zinaendelea.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.